BREAKING

Saturday 8 August 2015

TAMASHA LA SIMBA DAY LAWA KIVUTIO , SIMBA YAITANDIKA SC VILLA KIMOKO 1-0

   Kikosi cha SC Villa ya Uganda
  Mwinyi Kazimoto wakati wa kutambulishwa kwenye tamasha la Simba Day  


 Kocha wa Simba Dylan Kerry akikokota mpia katika mchezo wa Viongozi wa Simba dhidi ya timu ya wasanii,kocha huyo alifunga bao pekee
    Mashabiki wa Simba wakifuatilia mechi
 Wachezaji wa Simba wakitoka vyumbani kuingia Uwanjani
 Kocha Mkuu wa Simba Kerry akiwa na kocha Msaidizi Seleman Matola
   Hamis Kiiza'Diego' akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Villa
 Mussa Hasan Mgosi akiwa katika harakati za kugmbania mpira na beki wa Villla

SIMBA Dar es Salaam.

Simba inayonolewa na kocha kutoka Uingereza Dylan Kerr imeanza kuonyesha makeke yake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhi ya timu SC Villa ya uganda katika mchezo wa kirafiki uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Simba licha ya kucheza kandanda la kuvutia ilibidi wasubiri hadi dakika ya 89, ambapo Awadhi Juma ndiye aliyenogesha sherehe za Simba baada ya kufunga bao hilo kufuatia shuti kali alilopangua kipa wa Villa na mpira kumkuta Awadhi.

Awali ulifanyika mchezo wa Viongozi wa Simba na timu ya wasanii ambapo timu ya viongozi walipata bao 1-0 bao lililofungwa na kocha Mkuu wa Simba Kerr.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube