NAPE NNAUYE Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa.
NAPE NNAUYE Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa,wakti akizungumza na waandishi wa habari
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapindizi CCM, Taifa ambayo iliketi katika kikao chake cha jana,Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba Jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete,imemekamilisha kazi ya uteuzi wa wagombea Ubunge katika majimbo mawili ya Singida Mashariki na Kiteto
Akizungumza na waandishi wa habari Lumumba Jijini Dar es Salaam, Katibu wa Itikadi na Uenezi NEC Nape Nnauye, amesema kuwa wagombea Ubunge walioteuliwa kupeperusha bendera ya CCM, katika majimbo hayo ni pamoja na Jonathan Njau Singida Mashariki,na Emmanuel Papian John ambaye atapeperusha bendera ya jimbo la Kiteto.
Nape amesema kuwa kamati hiyo imezingatia mambo mbalimbali katika kuteua wagombea hao katika majimbo hayo, kwa lengo la kupata uongozi bora.
Aidha Nape amesema kamati hiyo imefanya uteuzi wa Kamati ya wajumbe 32 wa kampeni, kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu ambayo itaongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bwana Abdulrhaman Kinana, ambapo pia imewajumuisha baadhi ya wajumbe ambao walikuwa wagombea urais kupitia tikekti ya CCM, akiwepo Waziri wa Mambo ya Nje Bernad Membe, Januari
Makamba,Mwigulu Nchemba, Stephen Wasira,Razaro Nyalandu, na Makongoro Nyerere, wengine ni Vuai Ali Vuai kutoka Zanzibar, Shamsi Vuai Nahodha Zanzibar, na Seif Khatib.
No comments:
Post a Comment