BREAKING

Monday, 3 August 2015

TIMU YA TAIFA YA NGUMI YAREJEA NA MEDALI TATU ZA DHAHABU NA FEDHA

Timu ya taifa ya ngumi iliyokuwa mombasa katika mashindano ya East Africa Cities Club Championship , imerejea Tanzania huku ikiwa imetwaa medali tatu moja ya fedha na mbili za dhahabu.

Wachezaji wanne walishiriki katika mashindano hayo makubwa yaliyoshirikisha nchi za Afrika mashariki, pamoja na na nchi mwalikwa za Nigeria na Botswana, ambapo mabondia hao wameweza kufanya vyema katika mashindano hayo licha ya changmoto iliyokuwa nayo kabla ya maandalizi pamoja na fedha za kusafiri..

Wakizungumzia mashindano hayo nahodha wa timu ya taifa Said Hoffu pamoja na kocha wao Said Omary wamesema kuwa Tanzania imepata sifa kubwa kutokana mabondia hao kuonyesha kiwango kikubwa jijini Mombasa.

Wamesema kuwa iwapo Serikali itakuwa karibu katika mchezo huo timu hiyo ya Taifa ambayo itashiriki mashindano makubwa ya Afrika (All Africa Games), inaweza kufika mbali na kupeperusha bendera ya Taifa.

Naye Katibu Mkuu wa shirikisho la ngumi za Ridhaa, Tanzania (BFT),Makore Mashaga amesema kuwa timu hiyo imefanya vizuri na sasa wataiandaa zaidi kwa ajili ya mashindano mengine ya kimataifa


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube