BREAKING

Tuesday, 11 August 2015

TIMU YA MAJESHI YAKABIDHIWA BENDERA YA TAIFA TAYARI KWENDA UGANDA KUSHIRIKI MASHINDANO YA MAJESHI YA AFRIKA MASHARIKI

 Meja Jenerali wa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ, Simon Mumwi,akiwa na baadhi ya Maafisa wa Jeshi, wa JWTZ wakiwa katika ukakamavu kabla ya kukabidhi Bendera kwa timu
 Baadhi ya wachezaji wakitoa heshima kwa  Meja Jenerali wa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ, Simon Mumwi, katika hafla fupi ya kukabidhiwa bendera timu hiyo .Hafla hiyo ilifanyika Mbweni Jijini Dar es Salaam.
 Wachezaji wa timu za majeshi wakiimba wimbo wao maalum, katika hafla ya kukabidhiwa bendera kwa ajili ya mashindano.

 Wachezaji wa timu za Majeshi

 SIMON MUMWI-Meja Jenerali wa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ, akizungumza kabla ya kukabidhi bendera ya Taifa.

 SIMON MUMWI-Meja Jenerali wa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ, akikabidhi bendera kwa RICHARD MWANDIKE-Kiongozi wa msafara


Timu mya Majeshi imekabidhiwa bendera kwa ajili ya kwenda nchini Uganda kushiriki mashindano ya Majeshi    kwa nchi za Afrika Mashariki yatakayoanza kurindima Agosti 16mwaka huu.


Akizungumza wakati wa kukabidhi bendera timu hizo za jeshi Meja Jenerali wa Jeshi la wananchi Tanzania JWTZ Simon Mumwi, amewataka wachezaji hao kuzingatia suala la nidhamu michezoni pamoja na kujenga moyo wa uzalendo, kwa kuwa wanakwenda kuliwakilisha Taifa.

Aidha kwa upande wake kiongozi wa msafara huo Luteni Kanali Richard Mwandike, amesema wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanapeperusha vyema bendera ya nchi, kwa kuleta makombe mbalimbali kupitia timu zao.

Timu zilizoondoka ni pamoja na mpira wa miguu, Netiboli, riadha fupi na za nyika, mpira wa kikapu na mpira wa mikono.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube