Kufuatia mlipuko wa Ugonjwa wa Kipindupindu kutokea Jijini Dar es Salaam, baadhi ya wafanyabishara hususani wa Vitoweo,wamewaomba wafanyabiashara wengine kufanya usafi katika mabucha yao yanayouza nyama.
Mmoja wa wanyabiashara Saleh Seif Salum amesema kuwa ni vyema wafanyabiasha wa mabucha kuzingatia usafi ili kuepukana na madhara ya ugonjwa wa kipindupindu,ikiwepo kufanya usafi wa mara kwa mara na kuhakikisha inzi na wadudu wengine hawaingii kwenye mabucha.
Aidha ameiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya kufanya ukaguzi katika mabucha na wale wanaouza nyama nje ya bucha hasa wafanya biashara wadogo wadogo.
Hofu ya ugonjwa huo iliibuka jana baada ya watatu kufariki dunia na wengine 34 kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya mwananyamala na Mburahati jijini.
No comments:
Post a Comment