BREAKING

Saturday 8 August 2015

JK AFUNGUA BARABARA YA NDUNDU - SOMANGA YENYE UREFU WA KILOMETA 60 MKOANI LINDI

 Rais KIKWETE akizungumza wakati wa uzinduzi huo
waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli akipokelewa na Mkuu wa mkoa wa Lindi, Mh. Mwantumu Mahiza mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo Wilayani Kilwa Mkoani Lindi kushiriki ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa kilometa 60. Barabara hiyo imejengwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na ubahili wa mfuko wa Kuwait pamoja na mfuko wa OPEN.  
 
mgombea Urais wa Chama cha mapinduzi CCM Dkt John Pombe Magufuli akijitambulisha kwa wakazi wa mji wa Nangukurulu, mara baada ya sherehe fupi za ufunguzi wa barabara ya Ndundu-Somanga kukamilika Mkoani Lindi.
 Rais wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa pamoja  na mkewe Salma Kikwete wakimwagia maji mti wa Kumbukumbu walioupanda baada ya ufunguzi wa barabara ya Ndundu - Somanga Mkoani Lindi

 Rais KIKWETE akisalimiana na wananchi wakati wa uzinduzi huo
 Waziri wa Ujenzi Dkt. John  Pombe Magufuli akisalimiana na waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Marendengo., ambapo sherehe za uzinduzi wa barabara ya Ndundu - Somanga zilifanyika na Mgeni rasmi alikuwa Rais Dkt Jakaya Kikwete.


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube