Wimbi kubwa la baadhi ya wanachama na makanda kuhamia chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, ama ule muungano wa UKAWA, bado si tishio kwa Chama cha CCM, kutokana na mtaji walionao wa wanachama wao.
Nimefanikiwa kuzunguka Tanzania nzima nikiwa na dhamira nzuri yenye matunda kwangu, lakini kubwa nimefanikiwa kuambatana na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Ndugu Abdulrhaman Kinana, ambaye amezunguka nchi nzima kukagua ahadi za Uchaguzi Mkuu za Mwaka 2010, akiangalia utekelezaji wake, safari ambayo imetumika kwa miaka miwili,amekagua, amejenga, amesaidia japo penye kutoa msaada hakupenda aandikwe kwa kuwa ni jukumu lake binafsi.
Sikumshangaa sana, kwa kuwa tayari nilishamuzoea kwa kuwa tangu alipochaguliwa kuwa katibu Mkuu wa CCM, safari yake ya kujitambulisha ya kwanza kabisa ilikuwa ni Mkoa wa Mtwara, akiambatana na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Ndugu Nape Nnauye, ambaye Kinana mara nyingi humwita kiboko ya wapinzani, na hapo alionyesha kuwa anaweza kumsaidia mtu yoyote na asitake kusifiwa wala mkono wa kulia usifahamu alichotoa ni nini, huu ni mfano wa kuigwa kwa kuwa pia huyu ni Muumini mzuri wa dini ya Kiislamu, yenye maadili ya Heyeya (UTUKUFU)
Sitaki kumsifia sana na wala sitaki kuzungumza mengi ambayo nimekutana nayo nikiwa mmoja wa wandishi waliokuwa katika uso wake kumtafakari, ila hapa naeleza jinsi siasa ya Chama cha mapinduzi ilivyo kwa sasa, kuondokewa na wanachama ni juhudi za kupata wanachama wapya, na pengine siasa tunazoziona sasa ni zile za mjini tu tukienda Vijijini utakutana na umati mkubwa wenye nguo za Kijanani, hivyo Kinana na Nape wametengeneza wanachama wapya kwa staili ya kipekee Mikoani, na hata hawajatumia nguvu kubwa pengine hii tunaweza kuiita 'KUONDOKA KWA MAKADA WA CCM, KINANA, MAGUFULI, NAPE BADO WANAMTAJI KISIASA, NA MVUTO.....''
No comments:
Post a Comment