BREAKING

Sunday, 9 August 2015

MASHINDANO YA DANCE MIA MIA , WADHAMINI KAMPUNI YA SIMU ZA MKONONI VODACOM TANZANIA YAWAOMBA WASANII WAKUBWA KUCHUKUA VIPAJI.

   Washiriki katika shindano la Dance mia mia.
   Washiriki wa shindano la Dance mia mia wakicheza.
Baadhi ya majaji kutoka kulia Doreen, kati kati ni Sheta na Super Nyamwela wakifuatilia shindano hilo,Sheta alionekana kufurahishwa na baadhi ya washiriki hapa akishangilia.


Na Said Makala

Kampuni ya simu za mkoni ya Vodacom Tanzania imesema kuwa mashindando ya Dansi mia mia ,
yametoa frusa kwa vijana wengi nchini kufuatia wengi wa washiriki kuonyesha vipaji vyao.


Afisa Uhusiano wa vodacom Tanzania Matina Nkurlu amesema kama wadhamini wamefurahi kuona vijana wengi kuonyesha viwango vizuri ambapo amewaomba wasanii wakubwa wakiwepo wasanii kama Diamond , Ally Kiba na wengine kuwapa nafasi vijana hao wa kudance katika makundi yao ya muziki.

Matina amesema hayo wakati wa mashindano yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya leaders Club Jijini Dar es Salaam, ambapo amewaomba wasanii wakubwa kuwaunga mkono vijana hao.


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube