BREAKING

Wednesday, 19 August 2015

SINGLE MTAMBALIKE 'RICH' ASEMA WASANII WA FILAM WAMEKOSA UBUNIFU WANA COPY NA KU-PASTE

 Single Mtambalike, akizungumzia Ubunifu katika filam.

Imedaiwa Kukosa ubunifu na kutojiutuma kwa wasanii wakitanzania kuwa ni  chanzo kikubwa kinachopelekea kuzolota kwa  sanaa ya filamu na maigizo nchini kushindwa kufika ngazi ya kimatifa kama ilivo kwa baadhi ya nchi za afrika magharibi

Hayo yamesemwa na muogizaji mkongwe nchini Single Mtambalike maarufu kama "Rich " wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusiana  na fainali ya shindano la uibuaji wa vipaji  vya kuigiza itakayofanyika agost 22 mwaka huu katika ukumbi wa makumbusho ya taifa ulipo jijini Dar es salaam

Aidha Rich amesema kuwa wasanii wengi wakitanzania wamekuwa wakikosa wakilewa umaarufu walionao wakati huohuoi wakitungza filamu ambazo zimekuwa zikikosa utamaduni halkisi wa mtanzania

Kwa upande wao  kampuni ya Paisha  ambao ni wadhamini  wa shindano la hilo wamesema mshindi wa mwaka huu ataondoka na kitita cha shilingi milioni 50 pamoja na kuingia mkataba na  kampuni ya uuzaji na usamabzji wa filamu Proni Promotion limited.

 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube