BREAKING

Saturday, 15 August 2015

TANZANIA YABAINIKA KUWA NI MIONGONI MWA NCHI ZINAZOTOA HUDUMA BORA ZA USAFIRI WA ANGA -TATCA YANENA

   NANGWA MWITA Mwenyekti wa TACTA
   CHARLES CHAXCHA Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya Anga
 CHARLES CHAXCHA Mkurugenzi mkuu Mamlaka ya Anga, akisisitiza jambo

Imebainika Tanzania ni miongni mwa nchi zinazotoa  huduma bora za usafiri wa anga ukilingamnisha na nchi za ukanda wa afrika mashariki licha ya kukabiliwa na chanagmoto mbalimbali.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya usafirishaji wa anga Tanzania bwana Charles Chacha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa chama cha waongoza ndege nchini TATCA, amesema licha ya sekta hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali, bado sekta hiyo ina umuhimu mkubwa kutokana urahisi wake katika usafirishaji.

AIdha mkurugenzi huyo  amewataka wadau mbalimbali wa anga nchini kushiriki katika kuinua  uchangiaji wa sekta hiyo katika pato lataifa kuna kufikia aslimia moja.

Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha wongoza ndege tanzania TACTA Nangwa Mwita amesema chama hicho kimeweka mipango thabiti kwa kushirikiana na nchi jirani za kenya uganda na msumbiji ili kuimarisha umoja wa nchi hizo pamoja na kuongeza idadi ya wasafiri kwa kutumia anga.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube