BREAKING

Thursday 13 August 2015

VYAMA VINAVYOUNDA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI UKAWA CUF CHADEMA,NLD NA NCCR MAGEUZI WASAINIANA MAKUBALIANO YA KUPATA WAGOMBEA UDIWANI UCHAGUZI MKUU MWEZI OKTOBA.



 MAGDALENA SAKAYA Naibu Katibu Mkuu CUF,akizungumza na waandishi wa habari
                         JOHN MNYIKA Naibu katibu mkuu CHADEMA

  JOHN MNYIKA Naibu katibu mkuu CHADEMA,akifafanua jambo

Makatibu wa vyama vinne kutoka  Vyama vinavounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) vya CUF , CHADEMA ,NLD ,pamoja na NCCR MAGEUZI wakisaini makubaliano,yatakayowezesha kupata wagombea uongozi kupitia umoja huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi october katika ngazi ya madiwani.

Makatibu hao wakionyesha nyaraka waliosainiana makubaliano hayo.


Vyama vinavounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) vya Cuf , Chadema ,NLD ,pamoja na NCCRr Mageuzi vimeingia makubaliano yatakayowezesha kupata wagombea uongozi kupitia umoja huo kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi october katika ngazi ya madiwani.

Akizungumza nyakati tofauti wakati wa kusaini makubaliano hayo naibu katibu Mkuu wa chama cha wananchi Cuf  Bi Magdalena Sakaya, amesema lengo la makubaliano hayo ni kuhakikisha vyama vilivyopo ndani ya umoja huo wa katiba ya wananchi vinafanya vizuri kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Bwana John Mnyika amesema kuwa viongozi wa mbalimbali wa vyama vinavounda umoja huo wa katiba kwenye kata mbalimbali hapa nchini amewaomba kuheshimu makubaliano hayo kwa lengo la kuimarisha umoja wao.

Kwa upande wao kaimu katibu mkuu wa Nccr Mageuzi Dkt Geogre Kahangwa pamoja na Bw Tozzy Mahangwa ambae ni katibu mkuu wa chama cha  Nld wamesema wameridhia makubaliano hayo na wanaamini kupitia waraka huo huenda ikawa nafasi kwa umoja kuiongoza serikali ya Tanzania.
 

Umoja huo wa katiba ya wanachi ulianzishwa mnamo mwaka 2014 kwenye Bunge maalum la katiba hivi karibuni Ulimtangaza Waziri mkuu wa zamani bw Edward Lowasa kuwania nafasi ya urais kupitia umoja huo.   

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube