BREAKING

Wednesday 12 August 2015

KASEJA, MANYIKA WAZUMGUMZIA MAENDELEO YA SOKA, WASEMA TANZANIA NI MAARUFU IWAPO ITAWEKEZA MICHEZONI

    JUMA KASEJA akifafanua jambo katika mahojiano.

JUMA KASEJA akiwa anahojiwa


Makipa maarufu nchini waliowahi kutamba katika soka kwenye vilabu vya Simba na  Yanga pamoja na timu ya taifa Juma Kaseja pamoja na Peter Manyika wametoa wito kwa wadau soka nchini kuanzisha vituo kwa ajili ya kuzalisha wachezaji chipukizi hususani nafasi za makipa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mlinda mlango wa zamani Peter Manyika amesema kwa sasa amelenga kuibua na kuendeleza vipaji vya makipa ambao watatumika katika timu mbalimbali

Aidha Manyika ameongeza kuwa kituo chake kinajumla ya wanafunzi 36 ambao wanapata mafunzo huku akitoa nafasi kwa walinda milango wengine kujiunga na kituo hiko, ambapo amesema ni vyema wachezaji wa nafasi za walinda milango hao wakapatiwa mafunzo mazuri ili waweze kulisaidia taifa.

Kwa upande wake Juma kaseja ambae alikua hodari wa kuokoa mikwaju ya penati akiichezea timu ya Taifa Taifa Stars, Klabu ya soka ya Simba na Yanga mpaka kuwa maarufu na kupewa jina la Tanzania One amesemna Serikali pamoja na taasisi nyingne zinapaswa kuandaa miundo mbinu itakayoibua vipaji vipya, ambapo amewaomba wadau mbalimbali kumuunga mkono Manyika katika programu yake ya kuwaendelea vijna wenye vipaji.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube