MKURUGENZI WA DSTV TANZANIA MAHARAGE CHANDE AKIZUNGUMZA |
Tanzania kutetea ushindi ilioupata msimu uliopita
Ilboru, Al-Madrassat Ussaifiyatul Burhani zaongoza
Tanzania imepata wawakilishi wawili watakaoshiriki katika msimu wa saba wa tuzo maarufu barani Afrika kwa wanafunzi wapenzi wa masomo ya Sayansi naTeknolojia ijulikanayo
kama- DStv Eutelsat Star Awards. Wanafunzi hao Michael Ditrick wa shule ya Sekondari ya Ilboru – Arusha naTaher Rasheed wa Al-Madrasat Ussaifi ya Burhani y ajijini Dar es
Salaam
Michael ameshika nafasi ya kwanza katika uandishi wa insha maalumna Taher kwa mchoro maalum kuhusiana na sayansi ya Setelait ambapo wanafunzi zaidi ya 150 kutoka shule
mbalimbali nchini walishiriki katika mashindano hayo ya mwaka huu. Washindi hao walipatikana kutakana na utahini uliofanywa na jopo la majaji sita.
Kazi za washindi hao zimewasilishwa MultiChoice Africa ambapo zitapambanishwa na kazi kama hizo kutoka kwa washindi wa nchi nyingine kote barani Afrika na hatimaye
kupatikana mshindi wa jumla katika kila kipengele yaani wale walioandika insha na wale walioandaa mchoro.
Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande, amesema tuzo za mwaka huu zimekuwa na ushindani mkubwa ambapo shule kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo
Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Dodoma, Pwani zimeshiriki.
Kama kawaidatuzohizizinazawadikabambeambapomshindiwaInshaatapatafursayakuzurukituo cha EutelsatnchiniUfaransanapiakwenda Guiana kushuhudiamubasharaurushwaji wa
setelaitangani.
Mshindi wa bango atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini nakutembelea kituo cha anga cha nchi hiyo na pia makao makuu ya MultiChoice Africa akiwa kama mgeni
maalum.
Shulezitakazotoa washindi hao zitapata zawadi ya kufungiwa huduma ya DStvbure.
Wanafunzi wengine waliofanya vizuri katika mchakato huo ni pamoja na Pio Mwita wa UWATA Sekondari ya Mbeya ambaye ameshika nafasi ya pili kwenye insha na Peter Kiama
wa Feza Boys ya Dar es Salaam aliyeshika nafasi ya pili kwa upande wa bango.
Mwaka jana Tanzania iliibuka mshindi wa pili kwenye insha baadaya Davids Bwana wa FEZA Boys kunyakua nafasi hiyo nyuma ya mwanafunzi Leoul Mesfin kutoka Ethiopia.
No comments:
Post a Comment