BREAKING

Thursday 6 August 2015

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WANANCHI CUF PROF. IBRAHIM LIPUMBA , ATANGAZA RASMI KUJIUZURU WADHIFA WA UENYEKITI CUF.

M/kiti wa Chama cha wananchi Cuf ambaye pia ni m/kiti mwenza wa vyama vinavyounda Umoja vyama vya Katiba ya wananchi Ukawa Prof.Ibrahim Lipumba , amejiuzuru wadhifa wake wa kuongoza chama cha Wananchi Cuf leo.

Majira ya saa Nne na nusu Asubuhi Prof.Lipumba akiwa amefuatana na watu wawili ambao hawakutambulika mara moja , alifika katika hotel ya Peacock huku akiwa ameshika mkoba ukiwa na katiba iliyopo sasa na katiba iliyopendekezwa na kuanza kutoa historia ya kujiunga kwake na harakati za kukiongoza chama hicho mpaka hivi sasa.

Katika hali ambayo haikutarajiwa na waandishi wa habari katika mkutano huo, Prof.Lipumba alitangaza rasmi kujiondoa katika Uongozi wa chama hicho huku akieleza kuwa dhamira ndiyo inayomsuta, kutokana na kile alichodai kuwa viongozi walioingia katika ukawa, ndio wale waliokuwa wanapinga katiba Pendekezwa iliyoandaliwa na Jaji Joseph Warioba.

Hata hivyo Prof.Lipumba amesema ataendelea kubaki katika chama hicho na kuwa mwanachama wa kawaida ili kuendelea kutoa ushauri katika chama hicho.

Tetesi za kujiuzuru kwa Prof.Lipumba zilianza kuzagaa siku tatu zilizopita na kusababisha wapenzi na mashabiki wa chama hicho kufurika makao makuu ya Cuf Jana na kutaka kujua hatma ya Prof.Lipumba huku wakiimba nyimbo mbali mbali za kumsifu na kukisifu chama hicho....

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube