BREAKING

Friday, 7 August 2015

KURA MAONI YA CCM KUANGUKA KWA VIGOGO

 Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Dokta Benson Bana


Mhadhiri mwandamizi wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam Dokta Benson Bana, amesema kitendo cha Kuanguka kwa baadhi ya vigogo wa vyama vikubwa katika uteuzi wa wagombea nafasi za Udiwani,Ubunge na hatimaye Urais, inaashiria kuimarika kwa demokrasia ndani ya vyama husika.

Dokta Bana,katika sehemu ya pili ya mahojiano na mwandishi wa kituo hiki, yaliyojikita katika kutaka kujua maoni na mtazamo wake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu,amesema,hiyo ni dalili kuwa wananchi wa Tanzania ambao ndio wenye vyama, wanaweza kupima na kufanya tathmini ya kina kwa kumwangalia mgombea utumishi wake,uaminifu wake pale alipopewa dhamana ya kuwawaklisha wananchi.

Katika hatua nyingine, Dokta Bana, ameonyesha wasiwasi wake juu ya alichosema tabia iliyoota mizizi barani Afrika kwa baadhi ya wagombea katika chaguzi mbalimbali kutokubali matokeo kutokana kile alichosema kushindwa kujitathmini na kufanya utafiti iwapo wanakubalika ama la.

Wakati huo huo ,Dokta Bana,ameishukia taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini TAKUKURU, kwa madai kuwa inafanya kazi ya zimamoto ya kupambana na rushwa wakati huu wa uchaguzi,kufutia kile alichosema kuwa wanaojihusisha na vitendo hivyo walianza zamani.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube