BREAKING

Monday, 10 August 2015

AMGL YAKABIDHI MSAADA WA FEDHA KWA MTOTO JOACHIM JOSEPH KWA AJILI YA MATIBABU YA UGONJWA UNAOMSUMBUA WA MAPAFU KUSINYAA,NA MOYO

Mkurugenzi Uendeshaji wa AMGL waendeshaji wa vituo vya Channel Ten,DTV,  CTN na Redio Magic FM, Hamid Abdulrahman, akikabidhi msaada wa fedha taslimu shilingi laki tatu na sabini na nane elfu,kwa mama yake na mtoto Joachim Joseph anayesumbuliwa na ugonjwa wa moyo pamoja na Mapafu,msaada huo umetolewa na wanafuzni wanaosoma nchini Uholanzi ambao wanafuatilia channel ten kupitia mtandao wa channelten.co.tz

  Mkurugenzi Uendeshaji wa AMGL waendeshaji wa vituo vya Channel Ten,DTV,  CTN na Redio Magic FM, Hamid Abdulrahman akiwa na mama wa mtoto huyo Bi Felister Edwad.

 Mkurugenzi Uendeshaji wa AMGL akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada huo.

Baada ya   Kituo cha Channe ten kutangaza habari ya  mtoto Joackim  Joseph mwenye matatizo ya moyo na mapafu kusinyaa watu mbalimbai wameanza kujitokeza kutoa msaada kwa ajili ya mtoto huyo


Msaada uliotolewa na mwakilishi wa wanafunzi wanasoma nchini Uholanzi katika chuo cha WENGININGENI EPHRAHIM MUSHI ambapo anasema waliguswa na habari hiyo baada ya kuona habari ya channel ten kupitia mtandao

Akikabidhi msaada huo baada ya kuupokea msaada huo wa fedha taslim Mkurugenzi Uendeshaji wa AMGL HAMID ABDULRAHMAN amewashukuru watazamaji wa channel ten na kuhimiza kuendelea kusaidia jamii ya watu wenye mahitaji kama hayo ambapo na kuongeza kuwa watu wanaoishi nje ya nchi na wanaweza kupata habari zetu kupitia tovuti yetu ya www.channelten.co.tz.

Naye mama wa mtoto Joackim, Felister Edward ameshukuru kwa msaada huo na kusema kuwa hivi sasa ana matumaini mtoto wake atafanikiwa kufanyiwa operesheni  baada ya kupata fedha za kumfanyia vipimo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.

Mtoto  Joackim Joseph ambaye anasoma darasa la  nne katika shule ya msingi Chanika alianza kupata tatizo la kusinyaa mapafu mwezi wa tano mwaka huu baada ya kuugua 





No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube