Di Maria baada ya kutua Qatar kukamilisha uhamisho wake Paris Saint-Germain Jumapil.
Hatimaye Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina ANGELA DI MARIA amejiunga na klabu PSG ya ufaransa kwa dau la pauni milioni 44.4 baada ya kufaulu vipimo vya afya alivyofanyiwa na klabu hiyo mjini
Doha nchini Qatar.
Taarifa na sakata la kumpima mchezaji huyo wa zamani MANCESTER UNITED lililazimika kuchelewa
kufanyika baada ya madaktari kushauri mchezaji huyo aongezewe muda wa mapumziko ili mwili urejee katika hali ya kawaida baada ya kuwa safari ndefu ya kutoka Argentina hadi Qatar ilikokuwa klabu hiyo.
Awali Gazeti la the Daily mail liliripoti habari ya kocha wa United Louis van Gaal kutaka dau la mchezaji huyo liongezeke hadi kufikia pauni milioni 46.3 ambalo ni ongezeko la pauni milioni 3 ikiwa kama penati kufuatia mchezaji huyo kwenda Qatar bila ya ruhusa kutoka klabu yake ya Man U kuridhia kitu ambacho hata hivyo hakikufanyika.
No comments:
Post a Comment