BREAKING

Sunday, 16 August 2015

LOWASA NA WADHAMINI ARUSHA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa na Mkewe, Mama Regina Lowassa wakifanyia Ibada ya kimila na Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Mh. Edward Lowassa akipokea rungu maalum ikiwa ni ishara ya Uongozi, kutoka kwa Mzee Nyinyajwangwa Laiza, mara baada ya Ibada ya kimila na Wazee (Malaigwanani) ya Kimasai, wakati wa Mkutano wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
Mzee wa Kimasai (Laigwanani), Mzee Naftar Samson Mollel akiongoza ibada ya kimila na kumtambulisha rasmi kwenye ukoo, Mgombea Mwenza wa Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Dkt. Juma Haji Duni ambaye sasa anaitwa Juma Duni Ole Laiza.
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akizungumza na maelfu ya wananchi wa Jiji la Arusha, wakati akimtambulisha Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama hicho, Mh. Edward Lowassa, wakati wa Mkutano wa kutafuta udhamini wa Tume ya Uchaguzi na kutambulishwa kwa Mgombea huyo na Mwenza wake, Dkt. Juma Haji Duni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Kimandolu, leo Agosti 15, 2015.
Muasisi Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei akipena mkono na Mgombea Mwenza wa Urais wa UKAWA kupitia CHADEMA, Dkt. Juma Haji Duni.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa hadhara wa kutafuta wadhamini wa Tume ya Uchaguzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,pamoja na kutambulishwa kwa wananchi, uliofanyika Agosti 15, 2015, kwenye Uwanja wa Kimandolu, Jijini Arusha.
 Mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa, akihutubia wananchi.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube