BREAKING

Tuesday, 25 August 2015

MGOMBEA MWENZA WA URAIS MAMA SAMIA SULUH HASSAN ALIVYOPOKEWA MKOA WA KILIMANJARO,AIZITEKA WILAYA ZA TARAKEA,VUNJO NA MOSHI MJINI, ATAJA KIPAUMBELE ATAKAPOKUWA MAKAMU WA RAIS ASEMA ATAHAKIKISHA VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO VINAENDELEA KUPUNGUA KWA KASI, ATEMBELEA PIA HOSPITALI ZA UHURU..

 Wananchi wakiwa wanamsikiliza Mgombea Mwenza wa Urais Samia Suluh Hassan wakati alipokuwa akiwahutubia Moshi Mjini




 Mgombea Mwenza wa Urais Samia Suluh Hassan akihutubia


TARAKEA NA RONGAI-ROMBO

Mgombea mwenza kwa tiketi ya Chama cha mapinduzi CCM,Samia Suluh Hassan ,amesema kuwa Serikali ya awamu ya nne inayoongozwa na Rais Jakaya kikwete imefamefanya kazi kubwa katika sekta ya afya hususani kudhibiti vifo vya kina mama na watoto.


Bi samia ambaye yupo mkoani Kilimanjaro akiendelea na kampeni za urais akiwa ni  mgombea mwenza wa wa Mgombea Urais John pombe Magufuli mesema hayo baada ya kutembelea hospitali ya Huruma , iliyopo jimbo la Rombo, ambapo amesema kuwa hata wao watakapoingia Seikalini watahakikisha wanatekeleza kwa yale yaliyoachwa na serikali ya awamu ya nne, yakuhakikisha vifo vya mama na mtoto inakuwa historia kwa kuwa wataboresha sehemu za afya.


Katika hospitali ya Huruma , bi Samia pia alitembelea wodi za kinamama, na kuwapa pole, huku akihaidi kuwa Serikali inayokuja ya awamu ya tano itakuwa ya CCM, hivyo wasihofu waendelee kumuunga mkono kama mama jasiri aliyepata nafasi ya kuwawakilisha wanawake katika ngazi kubwa ya umakamu wa rais.


Baadae Bi Samia akaendelea na safari ambapo alifika Rongai na Tarakea, katika jimbo hili la Rombo na kuzungumza na wananchi, huku akiwahaidi vijana kuwapa kipaumbele katika kuwapa mitaji ili wajikombo katika umasikini.


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube