BREAKING

Friday, 21 August 2015

STARS KUELEKEA UTURUKI JUMAPILI



Kikosi cha wachezaji 22 kinachounda timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars' kinatarajia kuondoka nchini Jumapili wiki hii  kuelekea nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya mechi yake dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.

Akizungumza na waandishi wa habari  jijini Dar es Salaam,Afisa Habari wa Shirikisho la soka Tanzania TFF, Baraka Kizuguto amesema kuwa kikosi hicho kitaweka kambi ya wiki moja nchini Uturuki katika jiji la Estanbull pamoja na kucheza michezo miwili ya kirafiki ikiwemo dhidi ya Libya

Aidha kizuguto amesema kuwa timu hiyo itawakosa baadhi ya nyota wake watano wa kimataifa akiwemo mchezaji Mbwana Samata,Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa , Hassan Seif, Pamoja na mshambuliji Haji Yusuph.

Kikosi hicho cha kocha mzawa  Charles Boniface Mkwasa inakibarua kizito dhidi ya kikosi cha Nigeria chini ya kocha wake mpya Sunday Olise September 5 mwaka huu kwa jili ya kufuzu michuano ya AFCON.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube