Sunday, 13 September 2026
Saturday, 8 November 2025
BAADA YA KUJIONDOA KUGOMBEA NAFASI YA SPIKA KADA WA CCM ALEX MSAMA ASEMA DKT .TULIA NI MKOMAVU WA KISIASA...
Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mkurugenzi wa Msama Promotion Ndugu Alex Msama amesema ameona Watanzania wengi wakikosoa au kulaumu kitendo cha Dkt. Tulia Ackson kujiondoa kwenye michuano wa kugombea Uspika wa Bunge kwamba labda kuna kitu kibaya, au hatakiwi au amesusa.
Msama amesema kujitoa kwa Dkt. Tulia ni jambo zuri linaloashilia ukomavu wake wa kiuongozi na Kidemokrasia, amesema Dkt. Tulia hana kashfa mbaya, sio fisadi, sio mla rushwa bali ameonesha kwa vitendo ubora wake katika Uongozi hadi kuchaguliwa kuwa Rais wa Wabunge wote Duniani.
"Amewaachia nafasi wengine waweze kupata baada ya yeye kufanya vizuri katika kipindi chake, inaonesha hana tamaa na madaraka, na kwa uwezo wake mkubwa ni matumaini yangu kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan atamteua katika nafasi nyingine kubwa ili andelee kuwatumikia Watanzania' - amesema Msama.
Wednesday, 30 July 2025
BAADA YA JINA LAKE KUKATWA; ALEX MSAMA ATOA NENO
Siku moja tu baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kuondoa jina lake miongoni mwa watia nia wa Jimbo la Ubunge Ukonga jijini Dar, aliyetia nia, Alex Msama ametoa neno zito.
Msama ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Msama Promotions & Dira Media ametoa neno kwa kuwataka watia nia wote waliokatwa majina yao nchini kote kutoa ushirikiano kwa wale ambao majina yao yanakwenda kupigiwa Kura za Maoni ngazi ya kata na hatimaye kumpata mgombea mmoja atakayepeperusha bendera ya CCM kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025.
Huyu hapa Alex Msama: "Nilitia nia kuomba kuteuliwa na chama changu kugombea Ubunge Jimbo la Ukonga. Lakini isivyo bahati jina langu halikurudi.
"Siyo kwamba sifai. Nafaa ila jina langu halikurudi. Kwa wakati huu wamepatikana wengine ambao wamepewa nafasi na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama chetu ili kuendelea na mchakato.
"Sisi sote ni wana CCM. Kwa hiyo wote tuna sifa ila waliopitishwa wanafaa kwa sasa. Nawaomba watia nia wengine wote ambao pia majina yao hayakurudi, tuwape ushirikiano wale ambao majina yao yamerudi. Hiki ni kipindi cha kushikamana badala ya kusambaratika.
"Kwa hiyo niwaombe wale wote waliotia nia kama mimi lakini majina yao hayakurudi, tushikamane kwa nia ya dhati ya kuendelea kukiweka chama chetu katika umoja ili kumsaidia Mwenyekiti wa CCM-Taifa. Mama yetu, Rais Dkt Samia Suluhu Hassan."
Msama aliendelea kusema kuwa, katika kipindi hiki hategemei kuwepo kwa makundi kwa sababu ya majina yao kutorudi au kukatwa.
Akasema: "Kama watia nia wenzangu walimsikiliza vizuri Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Amos Makalla baada ya kumaliza kusoma majina yaliyorudi, alisema wote ambao majina yao hayakurudi tuwe watulivu bado chama kina mahitaji mengi. Kwa hiyo tutulie na kushikamana."
AZUNGUMZIA MAREKEBISHO YA KATIBA YA CCM HIVI KARIBUNI
Aidha, Msama alisema kuwa, wazo la viongozi wa CCM kuamua kurekebisha taratibu ya kurudisha majina mengi badala ya matatu kama ilivyokuwa awali ni wazo la busara na la maana sana.
Saturday, 1 March 2025
ROSE MHANDO :MSAMA NI BABA KWANGU ACHENI KUNIGOMBISHA NAYE.
Mwimbaji nguli wa Muziki wa Injili Afrika Mashariki na Kati, Rose Mhando amesema amekiri kwamba Mkurugenzi wa Msama Promotions ambaye ni mwandaaji wa matamasha mbalimbali ya Muziki wa Injili Alex Msama, ni zaidi ya Baba kwake kwani tangu alipoanza kazi zake za Uimbaji wa nyimbo za Injili amekuwa akifanya naye kazi kwa wema bila dhuluma na Msama hajawahi nidhulumu.
Friday, 21 February 2025
UPANDIKIZAJI WA MENO BANDIA KWA NJIA YA KISASA MUHIMBILI MLOGANZILA 45 KUNUFAIKA NA HUDUMA
Katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuboresha huduma za afya nchini Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imenza kambi maalum ya upasuaji wa upandikizaji wa meno bandia kwa njia ya kisasa kwa wagonjwa ambao wamepoteza meno yao kutokana na sababu mbalimbali.
Akizungumza wakati wa kambi hiyo Daktari Bingwa wa Afya ya Kinywa na Meno MNH.Mloganzila Dkt. Peter Shempemba amesema wagonjwa watakao hudumiwa katika kambi hiyo ni pamoja na wale ambao walifanyiwa upasuaji mwishoni mwa mwaka jana na wale ambao wanakuja kwa mara ya kwanza.
Ameongeza kuwa kundi la kwanza ni wale ambao walishawapandikiza mizizi ya meno katika awamu ya kwanza na kipindi hiki watapandikizwa meno na kundi lingine ni wale ambao wanapandikizwa mizizi kwa mara ya kwanza.
“Upandikizaji huu ni wa ubora wa hali ya juu, meno tunayoyapandikiza hayana tofauti na meno ya asili kwakuwa yanapandikizwa moja kwa moja kwenye mfupa wa taya na yanadumu kwa muda mrefu, hayawezi kutoka kirahisi, mtu ataweza kutafuna vizuri kama kawaida ” amesema Dkt. Shempemba.
Kambi hiyo inafanyika kwa kushirikiana wataalam wa ndani na Daktari Bingwa aliyebobea katika Upasuaji wa Taya kutoka Hospitali za Wochhardt Dkt. Chirag Desai ambapo itafanyika kwa kipindiki hiki cha siku saba kuanzia tarehe 20 hadi 26 Februari, 2025 ambapo takribani wagonjwa 45 watafanyiwa upandikizaji.
Thursday, 13 February 2025
UTEKAJI WA WATOTO MKUU WA MKOA WA MBEYA JUMA HOMERA AWATAKA WANAFUNZI WA HOLY LAND PRE- & PRIMARY SCHOOL KUKATAA LIFTI
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera akiteta jambo na Mmiliki wa Shuele ya HolyLand Pre-&Primary School Lawena Nsonda Baba Mzazi.
Tuesday, 4 February 2025
MSAMA ANG'AKA WAIMBAJI WA IN JILI KUPOTOKA MAADILI
Mkurugenzi wa Msama Promotions ndg Alex Msama Amewaonya waimbaji wote wa nyimbo za injili Ambao wamekuwa wakishiriki kwenye majukwaa na wasanii muziki wa kidunia, kwani kufanya ivo ni kushiriki kwenye kumtukuza shetani.
Pia amewataka wasanii hao kuacha tamaa ya pesa ambayo inawapelekea wasanii hao kwenda kushiriki kwenye majukwaa ya muziki wa kidunia,
“Nawaonya waache kushiriki madhabahu za shetani,2 Wakorinto 6: 14-18 Msiambatane pamoja na watu wasioamini, pia wajihadhari na kupenda pesa kwani pesa nyingine ni za maagano ya kuzimu” Alex MSAma
Alex Msama ni mdau mkubwa wa Muziki wa Injili na Hivi karibuni alipokea tuzo ya heshima ya kuwa muandaaji bora wa matamasha ya injili nchini Tanzania ambayo maarufu yalikuwa yanafahamika kwa jina la TAMASHA LA PASAKA









