BREAKING

Thursday 20 August 2015

MWANARIADHA MLEMAVU OSCAR PISTORIUS AHUKUMIWA KIFUNGO CHA NJE C

 
 
Michael Masutha ambaye ni waziri wa sheria nchni Afrika kusini amasema kuwa uamuzi wa kumuachilia mwanariadha huyo umechukuliwa mapema mno

Oscar Pistorius amekaa gerezani kwa muda wa miezi kumi baada ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp na alitarajiwa kuachiliwa ili atumikie kifungo chake cha nyumbani kuanzia kesho
 
Mwanariadha huyo mwenye ulemavu raia wa Afrika Kusini alipatikana na hatia ya mauaji ya mpenzi wake ambapo anatarajiwa kuwa huenda  akaachiliwa huru hapo kesho Agosti 21.

Kwa mujibu wa taarifa za idara ya magereza ya Afrika Kusini mwanariadha huyo aliyekuwa amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela huenda akasamehewa na kutumikia kifungo cha nje.

Oscar alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela katika kesi iliyovuta hisia kali kote  ulimwenguni ambapo inadhaniwa kuwa alimpiga risasi mpenzi wake akidai kuwa alidhani ni wezi wanaingia kwake katika siku ya wapendanao yaani Valentines Day

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube