BREAKING

Thursday, 20 August 2015

TIMU YA VIJANA CHINI YA UMRI WA MIAKA 15,KUANZA ZIARA BARANI AFRICA.

 Jamali Malinz akizungumza na waandshi wa Habari, wa kwanza kulia nai Ayub Nyenzi Mwenyekiti wa timu za Vijana.


 Timu ya soka taifa chini ya miaka ya 15 inatarajia kuanza ziara yake ya kimataifa barani Afrika mwezi desemba mwaka huu kwa ajili maandalizi ya kufudhu kwa michuano ya afrika chini ya miaka 17 itakatofanyika madagascar 2017.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Rais wa shirikisho la soka Tanzania Tff Jamal Malinzi amesema timu hiyo itaanza ziara yake mwishoni mwa mwaka katika nchi za zambia , Zimbabwe, Botswana pamoja na nchi za kusini mwa afrika

Aidha malinzi amesema kuwa Tff imeingia mkataba na kituo cha ukuzaji wa vipaji cha Alliance cha jjini mwanza kwa ajili ya kuwatunza vijana 20 waliopatikana kwenye mashindano ya taifa chini ya miaka 15.

Katika hatua nyingine malinzi ameeleza kuwa shirikisho hilo limewatafutia nafasi vijana watano kujiunga  na klabu maarufu ya Orlando Pirates inayoshiriki ligi kuu soka ya Afrika kusini.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube