Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete,wakati wa mazungumzo na mahojiano mafupi nyumbani kwake Msoga
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akitoka ndani kuelekea ilipo mifugo yake
Rais Kikwete akisikiliza jambo kwa makini
Hapa aneleza jambo kwa msisitizo
Rais Mstaafu Kikwete akiwa na Mkewe Mama Salma Kikwete, hapa ni kwenye zizi kubwa la Ng'ombe wake
DK Kikwete Akimshika Ng'ombe wake
Akifurahia jambo
Kikwete akisisitiza jambo kwa Mfanyakazi anayehudumia Ng'ombe
Dume likiwa linakula majani yaliyotengenezwa kisasa
Baadhi ya Ng'ombe wa Rais Mstaafu Kikwete
Rais Kikwete na Mkewe wakiangalia Ng'ombe wao
Ng'ombe akiwa anakunywa maji
Mfanyakazi akifanya usafi katika zizi la Ng'ombe
Baadhi ya Ng'ombe wakiwa mapumzikoni
Rais Mstaafu DK.Kikwete akionyesha Baadhi ya mabaki ya Chakula cha Ng'ombe
Rais mstaafu Dk.Jakaya Kikwete akieleza jinsi ufugaji wa Ng'ombe wake
Na Said Makala
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dk.Jakaya Mrisho Kikiwete, sasa ni mfugaji halisi baada ya kustaafu na kumkabidhi kijiti Dk John Pombe Magufuli, ambapo Kikwete amesema kuwa sasa anajikita katika ufugaji wa Ng'ombe pamoja na Kilimo.
Shamakala360 imemtembelea rais huyo mstaafu nyumbani kwake kijiji cha Msoga,Chalinze na kufanya naye mazungumzo kwa kina, kabla ya kutembezwa katika himaya yake ya ufugaji wa Ng'ombe.
Katika maswali kadhaa ambayo aliulizwa na mtandao huu, Rais Kikwete anaeleza amekuwa akifarijika zaidi kuona maendeleo mazuri ya ufugaji hivyo kustaafu kwake sasa nguvu anaelekeza katika Kilimo na ufugaji.
"Napenda Ufugaji kumbuka nimestaafu nimeamua kurejea Kijijini kwetu hapa Msoga kama unavyoona sasa nina Ng'ombe wengi sana nitaendelea kuwatunza na pia nitajikita kwenye Kilimo"Alisema
Katika mazungumzo hayo marefu pia Kiongozi huyo ambaye aliongoza Tanzania kwa Miaka 10, ameeleza kuridhishwa na kiwango kizuri cha Soka kinachoonyeshwa na nyota wanaosakata kandanda la kulipwa kunako klabu ya soka ya TP mazembe ya Kongo ambapo amesema ni wachezaji wenye nidhamu na ndio sababu inayowapa matumaini.
Kauli ya Kikwete imekuja baada ya nyota hao kufanikiwa kutwaa kombe la Klabu Bingwa Afrika dhidi ya timu ya USM ya Algeria na Samatta kutwaa kiatu cha dhahabu.
Aidha Rais huyo Mstaafu ameitakia kila la kheri timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa stars'inayotarajiwa kucheza mchezo wa kuwania kufuzu hatua za makundi ya kombe la Duni dhidi ya Algeria.
"Naitakia kila la kheri timu ya Taifa Stars,katika mchezo wao Jumamosi naamini wanaweza kuifunga Algeria,na wakasonga mbele hivyo nina imani kubwa kwao wanaweza kufika mbali hata mimi nilipokuwa rais nilikuwa na nia dhabiti kufikisha mbali soka, nashukuru hata hapa nilipofikia najua rais aliyenipokea kijiti Dk John Magufuli ni mpenda michezo naye ataendeleza yale niliyoyaacha" Alisema Kikwete.
Rais Kikwete atakumbukwa kwa mengi na wanamichezo kufuatia mikakati yake mbalimbali ya kuhakikisha soka linakua Tanzania ikiwepo kuleta makocha ambapo alilipa mishahara yake kama ilivyokuwa kwa kocha Mbrazili Marcio Maximo,si hilo tu bali hata sasa ameacha kumbukumbu baada ya kujenga kituo cha kuendeleza vipaji cha Kidongo chekundu Jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment