Moto Hauzimi na DStv, Star Life
nyumba ya Bollywood sasa ndani!
Kampuni
ya Multichoice inajivunia kuongeza chaneli
mpya ya filamu inayojulikana kwa jina la Star Life mahususi kwa ajili ya
wapenzi wa filamu na Tamthilia za
kihindi.
Chaneli
hii yenye maudhui ya kihindi inayorusha matangazo kwa Lugha ya kingereza
imeanza rasmi kupatikana tarehe 27 Agosti 2018 chaneli namba DStv 167 iliyopo
kuanzia kifurushi cha DStv Family.
Wateja
wa DStv na watanzania wote kwa ujumla wataweza kufurahia filamu nzuri na za Kisasa
za kihindi, Tamthilia na Series kali zenye kugusa hisia na tamaduni na maisha
ya kihindi na vipindi vingine mbalimbali vya burudani kupitia chaneli hii
vitakavyokuwa rushwa hewani kwa lugha ya kiingereza.
Kwa zaidi
ya miaka 20 chaneli hii imekuwa ikipeperusha bendera kwa kuwa chaneli
namba moja kutokana na ubora wa maudhui
ya filamu na sinema zilizosheni ndani
yake.
“Nyongeza ya chaneli hii ni matokeo ya kuhakikisha kuwa
wateja wetu wanaendelea kufurahia huduma za DStv kwa burudani za kisasa kabisa
ambazo hawatoweza kuzipata kwingine kokote. Chaneli hii itakuwa ikipatikana
ndani ya DStv kupitia chaneli namba 167 kuanzia kifurushi cha Family 39,000.Hakika Moto Hauzimi na DStv!
No comments:
Post a Comment