Ile tamthilia kabambe ya Huba inayoonyeshwa kupitia
DStv katika chanel ya Maisha Magic Bongo inaendela tena baada ya kumalizika kwa
msimu wa kwanza wa tamthilia hiyo mwezi Machi mwaka huu. Huu ukiwa ni msimu
pili, tamthilia hiyo ambayo imeainishwa kama moja ya tamthilia maarufu zaidi
ukanda wa Afrika Mashariki, imeanza kwa kishindo kutokana na kuongezwa kwa
vionjo na pia washiriki maarufu wa filamu hapa nchini.
Tamthilia ya Huba huigizwa hapa nchini na waigizaji
wa hapa hapa nchini akiwemo Rammy Gallis
(Dev), Riyama Ali, Muhogo Mchungu, Grace Mapunda (Tesa) na Aunt Ezekiel (jojo)
ambaye ni muigizaji mpya katika tamthilia hii.
Akizungumzia ujio wa msimu wa pili wa Huba, Mkuu wa
chaneli ya Maisha Magic Bongo Barbara Kambogi amesema tangu kuanza kwa tamthilia hiyo ya
Huba Mwezi Novemba mwaka jana imefanikiwa kuliteka soko la tamthilia hapa
Afrika Mashariki na kuifanya kuwa moja ya tamthilia matata kabisa katika soko
la Afrika Mashariki.
“Kwa mara ya kwanza katika historia ya filamu na
hususan tamthilila Watanzania tumefanikiwa kuiweka tasnia yetu ya uigizaji
filamu katika ramani ya kanda ya Afrika Mashariki na bara zima kwa ujumla
kutokana na ufanisi wa tamthilia yetu ya Huba ambayo inatayarishwa hapa nchini
na kuigizwa na watanzania wenyewe” alisema Barbara.
Amesema kuwa kwa ufanisi uloonyeshwa na tamthilia
hiyo katika msimu wa kwanza, wanatarajia kuwa msimu huu wa pili utakuwa wa
kuvutia zaidi hasa ikizingatiwa kuwa waigizaji wote wameiva visuri zaidi,
vionjo vimeongezwa na pia waigizaji wengine wapya akiwemo Anti Ezekiel ambaye
ni miongoni mwa waigizaji maarufu hapa nchini
“Sisi DStv, na hususan channel yetu ya Maisha Magic
Bongo, tulisikia kilio cha muda mrefu cha Watanzania wengi waliokuwa wakitutaka
kuongeza maudhui ya Kitanzania, na hatimaye tukaamua kuanzisha chaneli maalum
yenye maudhui kutoka Tanzania. Na sasa tunaendelea kuiboresha chaneli hii ya
Maisha Magic Bongo na maudhui yake kwa ujumla hivyo watanzania wasiache
kutazama chanel hii kwani ni yetu” alisema Barbara.
Tamthilia ya Huba katika chanel ya Maisha Magic
Bongo inapatikana katika vifurushi vyote vya DStv kikiwemo kile cha DStv Bomba
kwa shilingi 19,975 tu kwa mwezi kikiwa ni moja ya vifurushi vya bei nafuu
kabisa sokoni.
Msimu huu wa pili wa huba unatarajiwa kuendelea kwa
miezi kadhaa na tamthilia hiyo huoneshwa
katika chanel ya Maisha Magic Bongo (DStv 160) kila siku za Jumanne na Jumatano
saa moja na nusu usiku.
No comments:
Post a Comment