BREAKING

Wednesday 23 June 2021

RC MAKALLA AWAPONGEZA NMB KWA KUTOA MIKOPO KWA WATUMISHI.



Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amewataka Watumishi kukopa kwa malengo ya kuboresha maisha ya Sasa na baadae na kuhakikisha mikopo wanayochukuwa wanaitumia kuanzisha miradi yenye tija.

RC Makalla amewataka Walimu kuacha kurubuniwa kwa mikopo ya Chapu Chapu yenye riba kubwa ambayo mwisho wa siku inawaingiza Katika Maisha Magumu badala ya neema.

Aidha RC Makalla amewapatia Walimu somo la namna Bora ya kutumia Mshahara wao na kuweka akiba kwaajili ya kuanzisha miradi ya kujiimarisha kiuchumi ili watakapostaafu Waweze kuishi maisha Bora.

Hayo yote yamejiri wakati wa ufunguzi wa Semina ya Siku ya Walimu iliyoandaliwa na bank ya NMB.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube