MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho, Simba baada ya jana Juni 22 kumalizana na Mbeya City kwenye ligi wamekwea pipa leo Juni 23 kuelekea Songea.
Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes raia wa Ufaransa na msaidizi wake Seleman Matola, Juni 26 watakuwa na kazi ya kusaka nafasi ya kutinga hatua ya fainali ya taji hilo.
Ikiwa watashinda mbele ya Azam FC watakutana na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United v Yanga ambao utachezwa Juni 25.
Kwa mujibu wa Gomes amesema kuwa wanahitaji kuweza kutwaa ubingwa katika mashindano ambayo watashiriki.
"Tunahitaji kushinda na wachezaji nimewaambia kwamba ni muhimu kwetu kushinda hivyo nina amini kwamba tutapambana," amesema.
No comments:
Post a Comment