ENGLAND
TIMU ya Taifa ya England imefanikiwa kutinga Hatua ya 16 Bora baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Jmahuri ya Czech usiku wa jana Uwanja wa Wembley Jijini London.
Katika mchezo huo wa Kundi D, bao pekee la England limefungwa na nyota wa Manchester City, Raheem Sterling dakika ya 12 na kwa ushindi huo Three Lions inamaliza kileleni kwa pionti zake saba, mbele ya Croatia yenye pointi nne na zote zinafuzu 16 Bora.
Bahati mbaya kwao Czech wamezidiwa wastani wa mabao tu na Croatia, kwani nao wamemaliza na pointi tatu, wakati Scotland imeshika mkia kwa pointi yake moja.
No comments:
Post a Comment