SHIRIKA la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) linaisaidia
Tanzania kuwa na mfumo bora wa kukusanya na kuhifadhi taarifa za hewa ya ukaa
nchini ili taarifa hizo ziweze kutumika katika mipango mbalimbali ya kusaidia
kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi pamoja na kuwa na taarifa sahihi za
mchango wan chi katika kukabiliana na tatizo hilo.
Baadhi ya washiriki mafunzo hayo kutoka wizara mbalimbali na vyuo vikuu wakifuatilia mafunzo ya namna ya kutumia mfumo huo. |
Akizungumza na Waandishi wa habari wakati wa mafunzo kwa
wadau wakuu wa mpango huo na namna ya kutumia mfumo huo katika kukusanya
taarifa hizo mtaalamu wa miradi inayohusu nishati na mabadiliko ya tabia nchi
kutoka UNDP tawi la Tanzania Bwana Abbas Kitogo amesema mfumo huo utaiwezesha
Tanzania kuwa na takwimu sahihi za hali ya hewa ya ukaa na namna tunavyopambana
katika kuipunguza .
Ameongeza kuwa kwa sasa Tanzania hatuna taarifa sahihi na
rasmi sana pale inapotakiwa kueleza mchango wetu kama taifa katika kutatua
changamoto hiyo na hivyo kushindwa kujua kama nchi tufanye tuongeze nguvu wapi
au tufanye nini katika kusaidia jitihada hizo za dunia.
Aidha amebainisha kuwa kupitia mradi huo wa kujenga uwezo wa
serikali katika kujenga mifumo ya jinsi ya kuzia hewa ukaa Tanzania wameamua
kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali kama vile wizara na vyuo vikuu lengo likuwa
ni kuwawezesha wataalamu wa serikali kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa
zinazohusiana na mabadiliko ya tabia nchi na kuzitolea taarifa kule zinakotakiwa.
‘’Tunatakiwa kutoa taarifa kwa umoja wa mataifa ule mpango
maalumu wa hewa ukaa na mbadiliko ya tabia ya nchi tunazalisha hewa kiasi gani
na mipango yetu ya kupunguza ni kiasi gani na namna ambavyo kama nchi tunaweza
kupambana na tatizo hilo hivyo ni muhimu mfumo huu wa taarifa uwepo maana kwa
sasa hatuna’’ Alisema Kitogo.
Amesema kuwa Wataalamu wametungenezea mfumo GG inventory
System ambao utakuwa katika hali ya
taarifa lakini pia kama tovuti maalumu ambayo itakuwa inasimamiwa ofisi ya
makamu raisi lakini watakaokuwa wanaifanyia kazi ni kituo cha kitaifa cha
kufuatilia kaboni kilichopo Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA maana wao ndio wana utaalamu wa kufanya
kazi hii.
Ameongeza kuwa kwa kuweka mfumo huo SUA utawezesha wanafunzi
pia wanaosoma hapo kuweza kujifunza na kuwa na uwezo kuutumia mfumo lakini pia
kuona namna unavyofanya kazi pale ambapo watakutana nao.
Amesema kupitia UNDP wameweza kutafuta wataalamu hao na
kuwapa kazi ya kutengeneza mfumo huo na baada ya kuutengeneza sasa wameuleta na
kuwafonyesha unavyofanya kazi na kuwafundisha namna ya kuutumia maana ni mfumo
ambao unabadilika hivyo unahitaji kuboreshwa.
Kwa upande wake mratibu wa kituo cha kitaifa cha kufuatilia
hewa ya kaboni kilichopo SUA Prof. Zahabu Eliakimu amesema kuwa mwanzoni wakati
walipoanzsha kituo hicho cha kitaifa walikuwa wamejikita kwenye kufuatilia hewa
chafu zinazosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi walikuwa wanaiangalia zaidi
hewa moja ya kabondayoksidi lakini
kupitia mfumo huu watahusisha hewa zote saba zinazohusika katika kusababisha
mabariliki ya tabia nchi.
Amezitaja hewa hizo ambazo mfumo huu utahusika katika
kuzifuatilia ukiachia mbali ile ya carbondioxide ya awali ambazo zitaangaliwa
katika kila sekta kuwa ni Green house,Methane,Chlorofluorcarbon,Hydrofluorcarbon,Nitrous
Oxide,Walter Vapor pamoja na Ozone.
‘’Tunavyoenda na kuzingalia hewa zote hizi tunabaki kuona
kuwa hewa ambayo ndio inaongoza zaidi katika kuchangaia mabadiliko hayo ya
tabia ya nchi kuwa ni Carbondioxide lakini hizo nyingine zinachangia kwa kiasi
kidogo lakini sekta inayohusika zaidi ni sekta ya matumizi ya ardhi kwenye
mistu,kilimo makazi ya watu ndiyo
kupitia madaliko hayo’’ Alisema Prof. Eliakimu.
Kwa upande wake Mataalamu mwandamizi wa mazingira kutoka ofisi ya makamu wa rais Bi. Adelaida Tillya
amesema kuwa mfumo huo ni muhimu sana kwa taifa kwani utaisaidia nchi kuweka
mikakati thabiti ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi kwakuwa sayansi
imeonyesha vitu vinavyoweza kuachangia mabadiliko hayo na namna ya kukabiliana
nayo kama nchi na mtu mmojammoja.
‘’Tanzania inaonekana haichangii kwa kiasi kikubwa katika
mabadiliko ya tabia nchi kama ambavyo zinachangia nchi zingine, lakini ni
lazima kuangalia maendeleo ya nchi kama tunapunguza au tunaongeza uzalishaji wa
hewa ukaa’’ Alisema Bi. Tillya.
Ameongeza kuwa kwa nchi zinazoendelea zimejiwekea mikakati ya
kitaifa katika kuangalia malengo ambayo
nchi imejiwekea kama imefikiwa au la na kuweza kutoa ripoti kwa mamlaka husika kila
baada ya miaka miwili kama unavyotutaka Mkataba wa kimataifa tuliousaini wa kuungana na nchi zingine duniani katika
kupunguza tatizo hili.
No comments:
Post a Comment