BREAKING

Friday 6 April 2018

RAIS MAGUFULI AMTAMBUA MVUMBUZI WA TANZANITE MZEE JUMANNE NGOMA


[​IMG]

Mvumbuzi wa madini ya Tanzanite, Jumanne Ngoma akiongea na waandishi wa habari Dar es Salaam, katika moja ya siku ya maadhimisho ya miaka 46 toka ugunduzi wa madini hayo, Mkoani Arusha eneo la Merelani.

Mzee Jumanne Ngoma ndiye mvumbuzi wa madini haya, mwenye shahada ya Uvumbuzi alizotunukiwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maandhimisho ya sherehe za Mei Mosi Mbeya mwaka 1984.

Mzee Jumanne Mhero Ngoma (Mvumbuzi) wa madini haya ya Tanzanite, alizaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha Marwa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro.


Wazazi wake walikuwa wafugaji wa Ng'ombe na mbuzi hivyo waliishi maisha ya kuhamahama ili kupata malisho bora ya mifugo kama ilivyo hulka na tabia za wafugaji.

Wakati akiendelea na shule ya msingi, mwaka 1952 wazazi wake walihama kutoka Hedaru na kwenda kuishi Mererani. Mzee Jumanne Mhero Ngoma, aliweza kusafiri na wazazi wake hadi Mererani, akaendelea na masomo yake katika shule iliyokuwa ikiitwa Town School iliyopo Arusha mjini, ambako ilibidi akae na mjomba yake, Ruben Mkali aliyekuwa akiishi Arusha Mjini wakati huo.

Mwaka huo 1965, alifunga ndoa na Bi Fatma Mauya, na kupata watoto nane

Mzee Jumanne Ngoma alijiunga na kozi fupi ya madini iliyokuwa ikitolewa na Wizara ya Madini wakati huo. Baada ya kumaliza kozi ya madini katika ofisi ya madini Morogoro, Juni 1, 1966 alipata leseni ya madini baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Siku chache baada ya kumiliki leseni ya utafiti wa madini, Mzee Jumanne Mhero Ngoma alirejea nyumbani kwake Makanya.

Alipokuwa Makanya aliamua kuanza utafiti wake kijiji chake cha Makanya. Mzee Ngoma aliaza shughuli za utafiti wa madini, ndipo akagundua Madini ya Gypsum, na kuwa mtu wa kwanza aliyegundua Gypsum maeneo ya kijiji cha Makanya, sasa hivi eneo hilo linaitwa Chang'onko

Hivyo alipopata elimu hiyo ya madini aliamua kwenda Meralani, katika eneo la Lalouo kijiji cha Naisunyai kufanya utafiti wa yale mawe aliyoyaona wakati anachunga mifugo ya baba yake. Mwaka 1967 Januari, aliamua kuyapeleka mawe yale katika ofisi ya madini Moshi kwa uchunguzi. Alishauriwa na afisa wa madini kipindi hicho Bwana Bills, ofisi ya madini Moshi ikayapeleka kwenye maabara ya taifa Dodoma kwa uchunguzi zaidi.

Mnamo tarehe 23 Septemba 1967 maabara ya Dodoma ilithibitisha kuwa ni madini ya Zoisite ambayo kwa wakati huo hayakuwa na soko, lakini wakashauri huenda yakawa na soko siku zijazo.

Mnamo Mwaka 1984, Serikali ya Jamhuri ya muungano ilipotambua rasmi Mvumbuzi ya madini hayo na kuyapa jina la "TANZANITE" jina lililotokana na jina la nchi, yaani Tanzania na Zoisite na likapatikana jna hilo. Hapo alimtunukia cheti cha uvumbuzi katika sherehe ya siku ya wafanyakazi zilizofanyika mkoani Mbeya.

Kutokana na historia fupi hiyo mRais Magufuli amesema anafurahi kumtambua mzee ngoma kwa kuwa ndiye shujaa wa Tanzanite


Utambuzi huo ameutoa wakati wa kukabidhiwa Ukuta uliojengwa na Jeshi la Ulinzi Tanzania huko Mererani,Simanjiro


No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube