Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Kanda John Kasuku
Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akitoa maelezo kuhusu kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mara tu ya ufunguzi wa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo akitoa maelezo kuhusu kituo maalum cha huduma jijini Mwanza mara tu ya ufunguzi wa kituo hicho mwishoni mwa wiki.
Katika kuhakikisha kuwa inaimarisha
na kusogeza huduma zake karibu zaidi na wateja, kampuni ya MultiChoice Tanzania
imefungua kitua kipya cha huduma jijini
Mwanza.
Kituo hicho kilichofunguliwa mwishoni
mwa wiki ni muendelezo wa mkakati wa kampuni hiyo kuwasogezea wateja wake
huduma karibu ambambo hivi karibuni, kituo kama hicho kilifunguliwa mlimani
City jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa ufunguzi huo,
Meneja Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania Baraka Shelukindo amesema kituo hicho
ni cha Kisasa na kinaweza kuwapa wateja wa DStv huduma zote kuanzia kununua
vifaa, kufanya malipo, ufundi na huduma kwa wateja.
Amesema huu ni mkakati maalum wa
MultiChoice Tanzania kufungua vituo kama hivyo kote nchini ambapo hivi
karibuni vituo zaidi vitafunguliwa
katika miji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Dodoma.
Hivi sasa mkakati wetu mkubwa ni
kuhakikisha kuwa mteja aliyeko mkoani anapata huduma sawasawa na yule aliyepo
Dar es Salaam kwani vituo hivi vya huduma vimeboreshwa na kuwa na uwezo wa
kutoa kila aina ya huduma alisema Shelukindo.
Amewataka wateja wa DStv jijini
Mwanza kukitumia kituo hicho kwa ufanisi na pia sasa kampuni hiyo pia
inaimarisha timu yake ya mauzo, kuongeza idadi ya mawakala ili kuhakikisha kuwa
wateja wanahudumiwa kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa.
Kuhusu changamoto za kiufundi,
Shelukindo amesema hili sasa limepatiwa ufumbuzi kwani MultiChoice imetoa
mafunzo maalum ya ufundi kwa mamia ya vijana kote nchini kwa ajili ya
kuwahudumia wateja wake. Amesema kuanzia sasa kutakuwa na mafundi maalum
walioidhinishwa ambao wamepatiwa mafunzo maalum.
No comments:
Post a Comment