Wito
umetolewa kwa serikali kuhakikisha wanawadhibiti na kuwachukulia hatua za
kisheria wale wote watakaobainika wamebaka au kuwapa mimba wanafunzi wa shule
za Msingi na Sekondari nchini.
Baadhi ya wadau wa Elimu Wilayani Mvomero Mkoani Morogoro wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mkutano huo. |
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti wadau wa elimu wilaya ya mvomero mkoani Morogoro wakati wa
mkutano ulioandaliwa na mtandao wa elimu Tanzania TEN /MET ili kupeana mrejesho
wa namna ya kukabiliana na changamoto za mimba za utotoni kwa wanafunzi wa
shule ya msingi na sekondari.
Katika
mkutano huo wa wadau wamebaini ushiriki
wa karibu wa wazazi na watoto wao haupo kwa kiasi kikubwa jambo linaloelekea
kuendelea kuwepo kwa changamoto hiyo.
Kwa
upande wake afisa elimu wa wilaya hiyo Bi. Maajabu Nkamyemka amesema kwa wilaya
ya mvomero takwimu zinaonesha hadi April 6 mwaka huu takribani mimba 90
zimebainika kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambapo miongoni mwa
hizo mimba 13 ni kutoka shule za msingi.
Aidha
Bi. Nkamyemka amesema kuwa ni jukumu la wazazi na walimu kwa kushirikiana na
wanafunzi kuhakikisha wanawafichua wale wote ambao ni wahusika bila kuwafumbia
macho ili sekta husika kupambana nao ili kutokomeza janga hilo .
"kwa
kuwa binti akipewa ujauzito huwa tunahangaika tu na aliyempa ujauzito, na yule
mwenye ujauzito tunamuacha sasa bhas sasa kwa kuwa wazazi hawataki kuleta
ushirikiano tutamfungulia kesi mwanafunzi mwenye mimba pamoja na wazazi ili
wazaz wawachunge watoto wao ipasavyo "Alisema Nkamyemka.
Wadau hao wa elimu wakiwa ndani ya mkutano huo |
Naye
mratibu elimu wa kata za mhonda na Kweuma bwn, Heriamini Mariki amesema kuwa
kumekuwa na changamoto ya mimba hasa kwa wanafunzi, wa sekondari jambo ambalo
kwa kiasi kikubwa wazazi ndiyo chanzo cha tatizo hilo huku akitaja sababu
zinazochangia kuwa ni pamoja na uelewa finyu wa wazazi na wakati mwingine
umaskini kwa baadhi ya kaya nyingi wilayani humo.
“Sisi kama wadau wajibu wetu mkubwa ni
kuwapatia elimu wazazi juu ya athari za kutokaa karibu na watoto wao na kuwa
wawazi juu ya madhara ya kufanya ngono wakiwa na umri mdogo" alisema
Mariki
Naye
diwani wa kata ya mhonda Bw. Abdallah Hassani Khalifa ametoa rai kwa Serikali
kujenga hosteli kwa shule za kata ili kuondokana na tatizo la mimba za utotoni
linaloikumba nchi nzima kwa kiasi kikubwa, huku akiwataka wazazi na walimu
wanawapa watoto wanafunzi ushirikiano wa
kutosha na ulinzi kwani ndiyo haki pekee wanaotakiwa kuzipata ili kufanya vyema
katika masomo yao.
No comments:
Post a Comment