Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua majengo ya maabara za shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua nyumba ya walimu katika shule ya sekondari ya Kata ya Busonzo katika Kijiji cha Nampalahala, Leo 2 Aprili 2018.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakifatilia mkutano wa hadhara ukiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Nampalahala, Kata ya Busonzo wakati akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua ujenzi wa nyumba za madaktari wa kituo cha afya cha Uyovu akiwa katika ziara ya siku moja Wilayani Bukombe, Leo 2 Aprili 2018.
Na Mathias Canal, Geita
Mbunge wa Jimbo la Bukombe
Mkoani Geita ambaye ni Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko Leo 2
Aprili 2018 amechangia matofali 10,000 kwa ajili ya ukamilishaji Wa
vyumba vya maabara ili kurahisisha uanzisha Wa shule ya sekondari Kata ya Busonzo
Wilayani Bukombe.
Shule ya sekondari Busonzo
inahitaji kukamilisha maabara tatu ili iweze kufunguliwa ambapo serikali imetoa
milioni 40 kwa ajili ya kazi hiyo.
Mhe Biteko amechangia
matofali hayo Mara baada ya maagizo ya Waziri Mkuu Mhe Kassim
Majaliwa aliyoyatoa wakati Wa dhifa ya uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru
kwa mwaka 2018 katika uwanja wa Magogo mkoani Geita kwa kuwataka viongozi wa
mikoa ya Tabora, Geita, Mtwara na Shinyanga ambayo inaongoza kwa utoro wa
wanafunzi kwa shule za msingi na kwa sekondari wahamasishe umuhimu wa elimu na
mahudhurio endelevu shuleni.
"Mkoa wetu tumepata aibu
kubwa kwa kuwa namba mbili kwa utoro kati ya mikoa yote nchini, utoro huu hapa
wilayani kwetu unachangiwa na umbali wa kwenda shuleni, hapa Busonzo watoto
wetu wanasoma Runzewe ambapo ni mbali sana. Umbali huo unachangia utoro"
alisisitiza Mhe. Biteko
Katika sherehe hizo
zilizonakshiwa na Kaulimbiu ya mbio za mwenge kwa mwaka huu ambayo ni
‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’ Waziri
Mkuu alisema kuwa utoro wa wanafunzi wa Sekondari ni mkubwa zaidi kwa Mikoa
husika kuliko shule za msingi.
Mara baada ya uzinduzi Wa
Mwenge huo wa Uhuru kabla ya kuelekea Mjini Dodoma kwa ajili ya shughuli za
Bunge zinazotarajiwa kuanza kesho 3 Aprili 2018 Mhe Doto Biteko amezuru Kijiji
cha Nampalahala kilichopo Kata ya Busonzo na kujionea jinsi ujenzi Wa maabara
unavyoendelea.
Mara baada ya kubaini kuwa
kuna upungufu wa matofali 10,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo, Naibu
Waziri huyo amechagiza ujenzi huo kwa kuchangia gharama za ununuzi wa matofali
hayo ili ujenzi huo ukamilike kwa wakati.
"Mheshimiwa Waziri Mkuu
ameshatoa maelekezo ya kukomesha utoro naomba tukimbie kulitekeleza hilo na
ninaomba wazazi tuhakikishe watoto wote wanakuwa shuleni ni aibu mno sisi kuwa
vinara wa utoro". Aliongeza Mhe. Mbunge Na Naibu Waziri huyo.
Mhe Biteko amewaeleza wananchi hao jinsi ambavyo utoro kwa shule
za sekondari Mkoani Geita umekithiri jambo ambalo limepelekea Mkoa huo kushika
nafasi ya pili kwa utoro Kitaifa kwa asilimia 8.1, ambapo Mtwara imekuwa
nafasi ya tatu kwa asilimia 6.4, Shinyanga asilimia 6.3 huku nafasi ya kwanza
ikishikiliwa na Mkoa Wa Tabora kwa asilimia 9.7
Aidha, Mhe Biteko ameonyesha kusikitishwa na takwimu za Mkoa Wa
Geita kushika nafasi ya pili pia katika kwa utoro kwa shule za msingi kwa kwa
asilimia 3.1 nyuma ya Mkoa Wa Rukwa unaoongoza kwa asilimia 3.2
Aliongeza kuwa anatamani kuona
Wilaya ya Bukombe inahakikisha inafikia viwango bora vya elimu. Serikali ya
awamu ya tano inyoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli, imedhamiria kuboresha
elimu katika ngazi zote nchini, kuanzia Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu hivyo
wananchi wanapaswa kuitumia fursa hiyo kwa maendeleo ya wilaya hiyo na Taifa
kwa ujumla aliwaomba pia wananchi wa kata ya Busonzo kumuombea Rais
Magufuli na kuunga mkono juhudi za serikali.
No comments:
Post a Comment