BREAKING

Thursday 5 April 2018

TWIGA STARAS YAJITWISHA MZIGO MCHEZO WA MARUDIANO DHIDI YA SHEPOLOPOLO ,KATIKA MCHEZO WA KUFUZU KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWAKE AFCON BAADA YA SARE YA MABAO 3-3 UWANJA WA TAIFA

Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars, kimeshindwa kutumia vema Uwanja wake wa nyumbani katika mechi ya kwanza ya kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wanawake (AFCON) baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 dhidi ya Zambia 'The Shepolopolo'.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Stars walikuwa wa kwanza kuandika bao la kwanza kwenye dakikaya kwanza tu ya mchezo likifungwa na Stumai Abdallah.

Baadaye tena katika dakika ya 22, Twiga walijipatia bao la pili lililofungwa na Asha Rashid. Ilichukua takribani dakika 3 pekee bao la Twiga kudumu ambapo Barbra Banda aliweza kuifungia Zambia goli la kwanza kwenye dakika ya 25.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Stars walikuwa mbele kwa mabao mawili kwa moja.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikipambania kucheka na nyavu, ambapo mnamo dakika ya 46 tu ya mchezo Zambia walijipatia goli la pili kupitia Misozi Zulu na kuufanya ubao wa matokeo kusomeka 2-2.

Dakika moja baadaye tena Twiga waliandika bao la tatu likifungwa na Asha Rashid ikiwa ni dakika ya 47. Zambia walikuja kusawazisha tena katika dakika ya 79 ya mchezo kupitia Barbra Banda aliyefanya mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, matokeo yalikuwa 3-3.

Mtanange wa marudiano utafanyika baada ya wiki mbili zijazo Lusaka, Zambia.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube