BREAKING

Friday 13 April 2018

TANZANIA YAFANYA KWELI TUZO ZA KIMATAIFA ZA DSTV EUTELSAT STAR, MWANAFUZI ABEBA TUZO UGANDA


Tanzania imevunja rikodi kwenye Tuzo za kimataifa za wanafuzi zijulikanazo kama DStv Eutelsat Star Awards baada ya  mwanafunzi Taher Rasheed kutoka shule ya  Al-Madrasat Us-saifiyatul Burhaniyah ya Dar es salaam kushinda nafasi ya kwanza katika category ya poster(bango) baada ya mchuano mkali na mamia ya wanafunzi kutoka nchi zaidi ya 10 kote barani Afrika. 

Kwa upande wa insha mshindi alikuwa Amos Mumbere kutoka shule ya Ntare nchini Uganda

Tuzo hizi ambazo zinahusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango vyenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19 kote barani Afrika ambapo kampuni ya MultiChoice inaendesha shughuli zake.

Mwaka huu, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu manufaa yaliyoletwa na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku hapa ulimwenguni na ni jinsi gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli zote zinazofanyika kote duniani.


Taher alitangazwa rasmi jana jioni jijini Kampala nchini Uganda ambapo jopo la watahini maarufu lilikaa na kupitia kazi za wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za Afrika. Jopo hilo liliongozwa na Paolo Nespoli, mwanaanga nguli kutoka European Space Agency (ESA).

Akiongea baada ya kupokea habari hizo za ushindi, Taher amesema amefurahi sana kwa ushindi huo mkubwa ambao umemletea yeye, shule yake na taifa zima kwa ujumla sifa kubwa. “Nimefurahi sana kupokea taarifa hizi nzuri. Naamini ushindi wangu utakuwa ni chachu kubwa kwa wanafunzi wenzangu kote nchini kujitokeza kwa wingi na kushiriki katika tuzo kama hizi na mashindano mengine ya kitaaluma ya ndani na nje ya nchi,” alisema Taher.


Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande amesema wamefurahishwa sana na ushindi huo wa Tanzania katika mashindano hayo muhimu ya kitaaluma ya kimataifa. 

Chance amesema kuwa tuzo hizo zimeanzishwa kwa pamoja na MultiChoice Afrika na kituo cha anga cha Eutelsat huko Ufaransa kwa madhumuni makubwa ya kuwajengea wanafunzi ari ya kushiriki katika masomo ya sayansi na pia kuhamasisha ubunifu na ugunduzi katika tasnia ya sayansi. 

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube