Rais Dkt.John Pombe Magufuli amemwagia sifa kemkem Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF), Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dkt. Magufulu alisema, Rais mstaafu Kikete, amefanya mambo mengi makubwa nchini, katika nyadhifa mbalimbali alizoshikaserikalini na kwenye Chama Cha Mapinduzi (CCM).
“Mheshimiwa Kikwete, umefanya mambo makubwa kwa faida ya nchi yetu, katika nafasi mbalimbali ulizoshika ikiwemo kwenye chama, Jeshini, na hata ulipokuwa Rais, kwakweli unastahili pongezi nyingi”Alisema Rais Mahgufuli katika hotuba yake.
Alisema, Dkt. Kikwete ameimarisha uchumi wa nchi, kujenga demokrasia lakini pia kujenga mahusiano mema na nchi za nje.
“Hata mimi urais wangu kwa miasi kikubwa umetokana na msimamo wako, kwakweli ulinibeba na mimi nitakubeba sintakuangusha” alisema.
Awali akielezea madhumuni ya taaisi hiyo, iliyoanzishwa Februari mwaka 2017, Dkt. Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti, alisema, ni pamoja na kuleta mageuzi katika maisha ya watu hapa nchini Tanzania na kwingineko katika Afrika kwa kutoa majawabu yenye ubunifu, ya kweli kweli na endelevu kwa changamoto zinazowakabili wananchi
“Lakini pia dhima ya taaisi ni kushirikiana na serikali na wadau wengine katika kuleta mageuzi ya kimaendeleo katika katika ubora wa maisha ya watu katika Tanzania na kwingienko.” Alisema Dkt. Kikwete.
Akieleza zaidi Rais huyo mstaafu alisema, taaisi hiyo inalenga kufanya kazi katika Tanzania na Bara la Afrika (Pan Africa).
No comments:
Post a Comment