Timu ya Atletico Madrid imefanikiwa kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Real Madrid katika mchezo wa kuwania taji la Super Cup ya Ulaya usiku wa jansa huu Uwanja wa A. Le Coq Arena mjini Tallinn, Estonia.
Shujaa wa Atletico Madrid amekuwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Diego Costa aliyeipasua ngome ya Real Madrid mara mbili.
Costa alifunga bao la kwanza mapema tu dakika ya kwanza akimalizia pasi ya Diego Godin, lakini mshambuliaji Mfaransa, Karim Benzema akaisawazishia Real dakika ya 27 akimalizia pasi ya Gareth Bale.
Nahodha, Sergio Ramos akaifungia bao la pili Real Madrid kwa penalti dakika ya 63, baada ya Juanfran kuushika mpira kwenye boksi.
Coasta akarejesha matumaini kwa Atletico baada ya kuifungia bao la kusawazisha dakika ya 79 akimalizia pasi ya Muargentina, Angel Martin Correa na dakika 90 zikalazimika timu hizo zikiwa zimefungana mabao 2-2.
Saul Niguez Esclapez akaifungia Atletico Madrid bao la tatu dakika ya 98 akimalizia pasi ya kiungo Mghana, Thomas Teye Partey na Jorge Resurreccion Merodio, maarufu kama Koke akaifungia bao la nne timu hiyo dakika ya 104 akimalizia pasi ya Víctor Machin Perez au Vitolo kwa jina maarufu zaidi.
No comments:
Post a Comment