Klabu ya Barcelona kwa sasa ina matumaini tele kufuatia beki wake mahiri Gerard Pique kuanza mazoezi wakati wakielekea katika mchezo wao wa marudiano wa nusu fainali ya Kombe la Mfalme dhidi ya Athletico Madrid utakaopigwa usiku wa leo.
Beki huyo alilazimika kutolewa wakati wa mapumziko katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata Barcelona dhidi ya Athletic Bilbao Jumamosi iliyopita baada ya kupata majeruhi ya msuli.
Kocha wa klabu hiyo Luis Enrique amesema majeruhi hayo ya Pique yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na ratiba ngumu waliyonayo.
Hata hivyo, nyota huyo wa kimataifa wa Hispania alifanya mazoezi na wenzake jana kukiwa na kila dalili kuwa atakuwepo katika mchezo huo wa ambao Barcelona wanaongoza kwa mabao 2-1 waliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza.
No comments:
Post a Comment