Serikali ya imelitaka Shirikisho la Soka tanzania TFF kuwatumia waamuzi sahihi na wenye vigezo vya kuchezesha mechi kati yua Yanga na Simba Jumamosi wiki hii Mechi itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Michezo Yusufu Singo wakati akizungumza na wanahabari Jijini Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kuwa iwapo waamuzi hawatatenda haki upande mmoja basi huenda ilateta matukio mabao ya kimichezo kutoka na upenzi wa timu hizo na mashabiki wake.
Singo ametoa tahadhari akieleza pia kuwa Serikali imejipanga kuahakikisha mchezo huo unafanyika bila matatizo na mashabiki kutoleta matatizo kama yaliyotokea nyuma.
Kwa upande wake msimamizi wa Usalama wa Uwanja kutoka Jeshi la Polisi amesema wamejipanga vyakutosha kuhakikisha mchezo unamalizika salama.
Aidha viongozi hao waliwatembeza waandishi wa Habari kujionea mwenekano wa Uboreshaji wa Camera za Uwanja huo za CCTV zitakazooonyesha matukio yote sehemu za Uwanja huo, ambapo iwapo mashabiki wataleta fujo wataonekana moja kwa moja na kuchukuliwa hatua.
Simba na Yanga zinakutana kwenye Mchezo huo kila mmoja akitaka kupata pointi tatu mhimu na kujiwekea kileleni mwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania inayoelekea ukingoni.
No comments:
Post a Comment