BREAKING

Thursday, 23 February 2017

SERIKALI YAAHIDI KUUNGA MKONO JITIHADA ZOTE ZINAZOFANYWA NA WADAU WA MICHEZO NCHINI ZENYE LENGO LA KUENDELEZA SOKA LA VIJANA

Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye akizungumza wakati wa Uzinduzi huo

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo
Serikali imeahidi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wadau mbalimbali wa sekta ya michezo nchini, zenye lengo la kuendeleza soka la vijana na soka la wanawake nchini jambo litakalosaidia viwango vyake viendane na kasi ya ushindani kimataifa.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo wakati wa uzinduzi wa bodi ya mfuko huru utakaokuwa maalum kwa maendeleo ya soka la vijana na soka la wanawake, utakaokuwa na jukumu la kubuni vyanzo mbalimbali vya rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya timu hizo za taifa.

Katika hatua nyingine waziri Nape amewaomba wajumbe wa bodi ya mfuko huo kutekeleza makujukumu yao kama ilivyoainishwa kwenye katiba yake, huku akiwasihi watanzania kuiunga mkono bodi hiyo, jambo alilosema litasaidia soka letu kupiga hatua kutoka hapa lilipo.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube