Wachambuzi wa soka Uingereza wameendelea kumkosoa kocha wa timu ya Arsenal, Arsene Wenger kuwa kikosi chake kimekosa kiongozi wa Uwanjani na kupelekea kuendelea kufanya vibaya kwa kila mchezo ikiwepo Ligi Kuu ya Uingereza.
Gary Neville na Rio Ferdinand ambapo sasa wanafanya uchambuzi wa soka katika vituo vya televisheni Super Sport,wamesema kuwa mwalimu huyo anaheshima kubwa katika soka lakini anaangushwa na wachezaji wake ambao wameshindwa kupata kiongozi ndani ya uwanja tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma wakati wakiwepo wachezaji kama Thierry Henry, Vieira ,hodha Tony Adamsna Martin Keown ambao walikuwa wachezaji wenye kushimka kutokana na kuwaongoza wachezaji wengine kwa maslahi ya klabu na mashabiki wake.
Rio amenukuliwa akisema 'Moja ya sababu zinazoonekana kuisumbua Arsenal ni uongozi wa ndani ya uwanja. Si timu tena yenye watu ambao wakati mwingine kwa misemo ya wapenda soka huitwa Baba Mwenye Nyumba.
Rio amesema kuwa wakati Arsenal ilipokuwa chini ya nahodha Patrick Vieira,na Manchester United ilikuwa kwa Roy Keane timu hizo zilipokuwa zikikutana kila mchezaji walionyesha umhimu wa kuongoza Uwanjani.
Viera kwa upande wake anasema kuwa kwa sasa Manchester United ina kiongozi ndani ya uwanja japo sio nahodha lakini ni mchezaji mwenye kiwango kikubwa cha soka duniani, akimaanisha Zlatan Ibrahimovic kuwa hakuna mchezaji wa Man U anayeweza kubishana naye.
Viera anasema wachezaji wa Arsenal kwa sasa, kila mmoja ni mkubwa na hata wale nyota mahiri kama Mesut Ozil au Alexis Sanchez
No comments:
Post a Comment