BREAKING

Wednesday 15 February 2017

SERIKALI ZA TANZANIA NA JAPAN ZASAINI MKATABA WA KUJENGA UWANJA WA MPIRA WA MAGONGO WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 170.

Serikali za Tanzania na Japan zimesaini mkataba wa ujenzi wa uwanja wa mpira wa magongo maarufu kama Baseball utakaogharimu shilingi milioni 170 za kitanzania.

Akishuhudia zeozi la utiaji saini mkataba huo, Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo
 Nape Nnauye, amesema kuwa ni jambo kubwa la kujivunia kwani litakuwa ni hamasa tosha kwa maendeleo ya mchezo huo nchini na kufanya vijana wengi wenye vipaji kujitokeza kushiriki.

Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, amesema ni faraja kwa taifa lake kudumisha ushirikiano na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo michezo, lakini kwa ajili ya kuutunza uwanja huo amesema utakuwa chini ya usimamizi wa Shule ya Sekondari ya Azania na Chama cha Baseball Tanzania lengo likiwa ni kuhakikisha vizazi na vizazi katika taifa vinanufaika.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube