Roger Federa |
Roger Federer amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kushiriki michuano inayofanyika mjini Basel nchini Uswisi kila mwaka. |
Bingwa wa michuano ya tennis ya Australia kwa mwaka huu Roger Federer amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kushiriki michuano inayofanyika mjini Basel nchini Uswisi kila mwaka.
Kwa mujibu wa waandaji wa michuano hiyo kuongezeka idadi ya nyota wenye majina kunaipa michuano hiyo uzito.
Tangu aanze kushiriki michuano ya ndani kuanzia mwak 1998 Federer ameshinda mataji makubwa 7 ya kitaifa.
Federer mwenye miaka 35 amerejea katika mashindano ya mchezo huo mwezi januari mwaka huu ikiwa ni baada ya kukaa kwa kipindi kirefu kufuatia majeruhi.
No comments:
Post a Comment