Nchi ya Urusi imesimamishwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Riadha baada ya kubainika kuwa wanamichezo wake wamekuwa wakijihusisha na utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Hata hivyo, baadhi ya wachezaji wa Urusi wanaweza kushiriki na kushindana mahali popote endapo wanaweza kukidhi vigezo vya vipimo.
Kumbukumbu inaonyesha kuwa Urusi pia ilisimamishwa na shirikisho la riadha ulimwenguni IAAF mwezi Novemba mwaka 2015, na wanariadha wake kukosa kushiriki michuano ya Rio Olimpiki ya mwaka jana.
Uingereza wanatarajia kuwa wenyeji wa mashindano ya riadha ya dunia kati ya Agosti 04-13 mwaka huu.
Uamuzi wa kusimamishwa kwa Urusi umefanyika kupitia mkutano mkuu wa Baraza uliofanyika mjini Monaco.
No comments:
Post a Comment