Monday, 27 February 2017
Sunday, 26 February 2017
SIMBA NI ILE ILE NA MASHABIKI NI WALE ALEEEEEEE, YAITANDIKA YANGA BAO 2-1 NA KUJICHIMBIA KILELENI MWA LIGI
Mshambuliaji wa Simba Laudit Mavugo akitafuta njia ya kumtoka Beki wa Yanga Kelvin Yondan
|
Beki wa Simba Janvier Besala Bukungu akichuana vikali na kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima. |
Shuja wa Simba aliyefunga bao la Ushindi Shiza Ramadhan Kichuaya akiwa amenyanyuliwa na Menmeja wa Simba Mussa Hassan Mgosi, baada ya kufunga bao. |
12:10
MBUNGE RITTA KABATI KUSAIDIA UJENZI WA OFISI TATU ZA CHAMA CHA MAPINDUZI MANISPAA YA IRINGA
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akimkabidhi mifuko ya saruji kwa ajiri ya ujenzi wa jengo la ofisi ya chama katika kata ya Ruaha kwa mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa katika eneo la uwanja wa kujenga ofisi ya kata ya Ruaha
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akibadilishana mawazo na katibu wa ccm manispaa ya Iringa Nuru Ngereja
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wanachama wa hama hicho wa kata ya ruaha
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) akiwa na
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza pamoja na viongozi wengine wa chama hicho.
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati akipokelewa na wanachama wa mtaa wa kigamboni mkoani Iringa
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Iringa Ritta Kabati kupitia chama cha mapinduzi (CCM) ameanza kusaidia Ujenzi wa ofisi za Matawi ya CCM katika kata mbali mbali za Jimbo la Iringa mjini kama sehemu ya majukumu yake ya kukijenga chama hicho ambacho kilipoteza kiti cha ubunge na halmashauri kuchukuliwa na wapinzani.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mifuko ya saruji kwa Ujenzi wa ofisi za Tawi Kigamboni na Ruaha ,Kabati alisema kuwa anafanya hivyo kama njia ya kutekeleza ilani na maadhimio ya miaka arobaini ya chama cha mapinduzi.
“Nakipenda chama changu ndio maana napigana sana kuhakikisha chama cha mapinduzi mkaoni mhapa iringa kinarudi mahala pake na kuhakikisha kinaaminika kwa wananchi na wanachama wa manispaa ya Iringa”.alisema Kabati
Hata hivyo Kabati alisema kuwa ataendelea kusaidia Ujenzi wa ofisi hizo ili kuona ndani ya kipindi kifupi cha miezi mitatu ama sita kila tawi linakuwa na ofisi yake ya tawi na aliwataka wanachama wa CCM kushikamana na kuendelea na Ujenzi wa ofisi hizo pamoja na kujihusisha na shughuli nyingine za kijamii
"Haiwezakani chama kikubwa kama hiki kukosa ofisi za matawi wakati tunamaeneo mengi ya kujenga ofisi nitakikisha tunashirikiana na wanachama na wananchi wengine kujenga hizo ofisi ili kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DR John Pombe Magufuli ambaye anapambana kuhakikisha cha mapinduzi kinakuwa chama cha wananchi wa chini na sio matajiri pekee yao".alisema Kabati
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi(CCM) manispaa ya Iringa Abeid Kiponza aliwataka wanachama kuwa kusahau yaliyopita na kuanza kujenga chama upya.
“Tulipoteza halmashauri ya Iringa na jimbo hivyo inabidi tukae chini na tujipange upya kukijenga chama maana tunajua kwa kujenga ofisi za matawi zitatusaidia kurudisha hadhi na hali ya chama hapa manispaa kwa kutoa huduma bora kwa wananchi wote bila kuchagua chama”.alisema Kiponza
Kiponza alimshukuru mbunge wa viti maalumu Ritta kabati kwa mchango anaoutoa kwa kuleta maendeleo katika manispaa ya Iringa hasa ukiangalia ujenzi wa majengo mbalimbali ya shule,taasisi za kidini,taasisi za kijamii hapa kujenga majengo ya chama.
Lakini Kiponza alimtaka mbunge Kabati kuwasaidia wananchi wanaodhurumiwa na kunyang’anywa mali zao katika manispaa ya Iringa.
“Hapa kigamboni kunawananchi wanapigwa na viongozi wa mtaa kwa kuwa wapo CCM tu na wamenyang’anywa kituo cha kuchotea maji ambacho kilikuwa mradi wa chama cha mapinduzi hivyo lazima upambane kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na mali za chama zinarudi kwenye chama”.alisema Kiponza
Naye Katibu wa CCM manispaa ya Iringa Nuru Ngeleja alisema kuwa wamejipanga kuhakikisha ofisi zote za chama zinajengwa na zinakuwa katika ubora unaotakiwa kutokana na ukubwa wa chama cha mapinduzi(CCM) na kuahidi kuwa wataendelea kumuunga mkoano Rais wa jamhuri ya muungano ya Tanzania Dr John Pombe Magufuri.
“Sisi tunafanyakazi ya kumsaidia mwenyekiti wetu wa chama ambaye ni Rais wetu kwa kufanya kazi na kuisimamia serikali kufanya kazi kwa uhakika na kuwafaikia na kuwatumikia wananchi waliowaweka madarakani mpaka sasa”. Alisema Ngereja
11:43
Thursday, 23 February 2017
SERIKALI YAAHIDI KUUNGA MKONO JITIHADA ZOTE ZINAZOFANYWA NA WADAU WA MICHEZO NCHINI ZENYE LENGO LA KUENDELEZA SOKA LA VIJANA
Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Nape Nnauye akizungumza wakati wa Uzinduzi huo |
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Nnauye akisisitiza jambo |
Hayo yamebainishwa na Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo wakati wa uzinduzi wa bodi ya mfuko huru utakaokuwa maalum kwa maendeleo ya soka la vijana na soka la wanawake, utakaokuwa na jukumu la kubuni vyanzo mbalimbali vya rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya timu hizo za taifa.
Katika hatua nyingine waziri Nape amewaomba wajumbe wa bodi ya mfuko huo kutekeleza makujukumu yao kama ilivyoainishwa kwenye katiba yake, huku akiwasihi watanzania kuiunga mkono bodi hiyo, jambo alilosema litasaidia soka letu kupiga hatua kutoka hapa lilipo.
16:52
NAMAINGO BUSSINESS AGENCY NA NHIF YAWAKUTANISHA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA TANGA
JA wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga (NHIF) Ally Mwakababu akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wajasiriamali na Taasisi ya Kibiashara ya Namaingo Bussiness Agency uliokuwa na lengo la kuwahamasisha kujiunga na bima ya Afya na kuhalalisha biashara zao |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Bi Ubwa Ibrahima akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wa wafanyabiashara na wajasiamali mkoani Tanga leo |
Mkurugenzi wa Kampuni ya Namaingo Business Agency, Bi Ubwa Ibrahim akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wa pamoja. |
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa
Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akifafanua namna
ya wajasiriamali na wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na huduma
mbalimbali ikiwemo za matibabu kupitia mfuko huo
Afisa Matekelezo wa
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akifafanua namna ya wajasiriamali na
wafanyabiashara wanavyoweza kunufaika na huduma mbalimbali ikiwemo za
matibabu kupitia mfuko huo ikiwemo kufanya biashara zinazotambulika
kisheria ili kuisaidia serikali kupata mapato
Baadhi ya wafanyabiashara
na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia
mkutano huo
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akimsikiliza kwa umakini mmoja wa wafanyabishara waliojitokeza kwenye mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Police Mess mkoani Tanga
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoani Tanga(NHIF) Miraji Kisile akisistiza jambo katika mkutano huo kwa baadhi ya wafanyabiashara namna wanayoweza kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kwa ajili ya kupata matibabu
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo
Baadhi ya wafanyabiashara na wajasiriamali kutoka maeneo mbalimbali mkoani Tanga wakifuatilia mkutano huo Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
16:29
Wednesday, 22 February 2017
NAPE KUZINDUA MFUKO WA KUSAIDIA SERENGETI BOYS
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Nape Nnauye |
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa miguu kwa vijana na wanawake.
Uzinduzi huo utakaofanyika saa 5.00 asubuhi, utahudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Mkurugenzi wa Michezo, Yussuph Singo. Utafanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Courtyard, Upanga jijini Dar es Salaam.
18:00
ROGER FEDERER ASAINI MIAKA 3 KUCHEZA MASHINDANO YA NDANI USWISI
Roger Federa |
Roger Federer amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kushiriki michuano inayofanyika mjini Basel nchini Uswisi kila mwaka. |
Bingwa wa michuano ya tennis ya Australia kwa mwaka huu Roger Federer amesaini mkataba wa miaka mitatu wa kushiriki michuano inayofanyika mjini Basel nchini Uswisi kila mwaka.
Kwa mujibu wa waandaji wa michuano hiyo kuongezeka idadi ya nyota wenye majina kunaipa michuano hiyo uzito.
Tangu aanze kushiriki michuano ya ndani kuanzia mwak 1998 Federer ameshinda mataji makubwa 7 ya kitaifa.
Federer mwenye miaka 35 amerejea katika mashindano ya mchezo huo mwezi januari mwaka huu ikiwa ni baada ya kukaa kwa kipindi kirefu kufuatia majeruhi.
17:49
JUMA KASEJA BADO ANAKIMBIZA, ACHAGULIWA KIPA BORA MWEZI JANUARI....LIGI KUU BARA
Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania TFF Alfredy Lucas amezungumzia jinsi nyota huyo alivyoibuka mchezaji bora.
17:40
Tuesday, 21 February 2017
MAJALIWA AWASALIMIA WANANCHI WA BASHNET AKIWA KWENYE ZIARA ZAKE
Monday, 20 February 2017
MAJALIWA AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA MBULU
Subscribe to:
Posts (Atom)