BREAKING

Monday, 30 January 2017

MABINGWA WA AFRIKA KLABU YA MAMELODI SUNDOWNS WATUA NCHINI, KUUMANA NA SIMBA PAMOJA NA AZAM FC




Klabu Mabingwa  wa Afrika, Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini wametua jijini Dar es Salaam, kwa ziara ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya vigogo wa Tanzania, Simba na  Azam FC .

Timu hiyo imewasili ikiwa na msafara wa takribani watu 50, ambapo 25 miongoni mwao ni wachezaji ambao watasakata kandanda na timu hizo za Simba na Azam FC.

Kocha Mkuu wa timu hiyo Pitso Mosimane, pamoja na Nahodha Hlompho Kekana,wamesema ujio wao ni kwa ajili ya kujiandaa na msimu wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi hivi karibuni.

Wamesema kuwa wanaamini timu hizo zinaushindani mkubwa kisoka hivyo watapata mazoezi ya kutosha katika micvhezo hiyo miwili.

Mchezo wa kwanza utachezwa Februari 1 na wa pili utakuwa Februari 3 mwaka huu katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube