Mavugo
MAPINDUZI
Na Mwandishi wetu Scolastica -Zanzibar
Ni simba na Yanga Jumanne zitachuana katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi, huko Visiwani Zanzibar kwenye Dimba la Aman.
Watani hao wa jadi watamenyana huk wakiwa na kumbukumbu ya sare ya kufungana mabao 1-1, katika mchezo wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa kwanza.
simba imefika katika hatua hiyo baada ya kuifunga Jang’ombe Boys, mabao 2-0 huku shujaa akiwana ni Mrundi Laudit Mavugo aliyefunga mabao yote.
Mchezo huo utafanyika Jumanne Saa 2:15 usiku Uwanja wa Amaan, Zanzibar katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar timu hizo zinakutana kutokana na Simba kuongoza katika kundi lake la A kwa pointi zake 10, ikifuatiwa na Jang’ombe Boys,huku Yanga wao wakishika nafasi ya pili katika kundi lake,lililoongozwa na Azam FC.
No comments:
Post a Comment