Kiungo wa Leicester city Riyad Mahrez ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika wa mwaka.
Mahrez
mwenye miaka 25 raia wa Algeria aliyeisaidia Leicester kushinda taji la
ligi kuu soka England msimu uliopita, tiyari ameshinda tuzo ya mchezaji
bora wa England sambamba na mchezaji bora wa BBC AfrikaMshambuliaji wa Senegal na klabu ya Liverpool Sadio Mane na mshambuliaji wa Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Gabon Pierre-Emerick Aubameyang walikuwa wakiwania tuzo hiyo pia.
Mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Nigeria Alex Iwobi ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi.
Denis Onyango wa uganda na klabu ya Memelodi Sundowns akishinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ligi za ndani.
Mchezaji bora kwa kina dada imeenda kwa Asisat Oshoala wa Liverpool na timu ya taifa ya Nigeria huku timu bora ya mwaka ikiwa ni Uganda.
No comments:
Post a Comment