BREAKING

Wednesday, 11 January 2017

DIAMOND KUWACHEZESHA CHAMBUA KAMA KARANGA WANASOKA GABON,NI KATIKA UFUNGUZI WA FAINALI ZA AFCON,SERIKALI,DSTV WATIA UBANI

Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akizungmza kabla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa Mwanamzuziki Nasib Abdul ,na Kundi la WBC linalokwenda Gabon kwa ajili ya kutumbuzi kwenye ufunguzi wa Fainali Januari 14 Mwaka huu

Waziri Nape akimsikiliza Diamond akizungumza katika hafla ya kuagwa kwenda Gabon







Waziri Nape akimkabidhi Bendera ya Taifa Mwanamzuki Diamond tayari kwa Safari ya kwenda Gabon kutumbuzi kwenye Ufunguzi wa Fainali za AFCON Januari 14 DSTV Tanzania wamedhamini tiketi za wasanii wote








Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye, amemkabidhi bendera ya Taifa Msanii Nasibu Abdul Maarufu kwa jina la Diamondi tayari kwa kwenda nchini Gabon kwa ajili ya kutumbuiza katika ufunguzi wa Fainali za Mataifa ya Afrika AFCON yanayotarajiwa kuanza Januari 14 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Multichoice Tanzania Waziri Nape amesema kuwa Serikali imefurahishwa na kitendo cha msanii huyo kualikwa kutumbuiza katika michuano hiyo mikubwa jambo ambalo linaitangaza Tanzania kwa njia nyingine tofauti na soka baada ya timu ya Taifa kushindwa kufanya vyema.

Nape amelitaka kundi zima la WCB kwenda kuwakilisha vyema katika ufunguzi huo huku akiusifu uongozi wa Multichoice kupitia DSTV kwa kugharamia udhamini wa tiketi wa kundi zima akiwasema ni moyo wa kizalendo.

"Imeelezawa pia katika kuhakikisha watanzania wengi wanashuhudia mashindano hayo DSTV imeyaweka kwenye channel ya Supersport ambayo ipo katika kifurushi cha Bomba ,moja ya vifurushi vya bei nafuu"

Naye Balozi wa DSTV Tanzania Lucas maarufu kama JOTI, amewaomba watanzania kuhakikshi hawakosi kutazama ufunguzi huo ambao msanii Diamond atatumbuiza pamoja na kundi lake la wasafi WBC, pamoja na kununua vifurushi vya Bomba,

No comments:

Post a Comment

 
Copyright © 2016 Shamakala
Designed by Switch International | SHAMAKALA 360
    Twitter Facebook Google Plus Vimeo Videosmall Flickr YouTube